Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Evra amtaka Suarez wapigane

Muktasari:

  • Mfaransa huyu amekuwa akijifua katika michezo ya mapigano tangu mwaka 2016 akiwa pamoja na nyota mwenzake kutoka Ufaransa Cedric Doumbe.

MANCHESTER, ENGLAND: LEJENDI wa Manchester United, Patrice Evra, yupo kwenye mchakato wa kufanya mabadiliko ya kushangaza kwa kuwa mpiganaji wa MMA  na anataka kucheza pambano moja dhidi ya Luis Suarez.

Mfaransa huyu amekuwa akijifua katika michezo ya mapigano tangu mwaka 2016 akiwa pamoja na nyota mwenzake kutoka Ufaransa Cedric Doumbe.

Akizungumzia mchezo huo, Evra mwenye umri wa miaka 43 alisema: “Mnajua kwa sasa napenda mchezo huu pia! Nimecheza katika viwanja vikubwa duniani, nimeshinda makombe yote makubwa katika soka, lakini usiku wa pambano langu la kwanza wa PFL Europe Paris utakuwa wa kipekee sana kwangu. Nimekuwa nikijifua na mabingwa wa dunia kwa miaka mingi na wao pia wanajua niko tayari kwa hili.

Nitatoa burudani kubwa katika ukumbi wa Accor Arena Mei 23, hivyo njooni kushuhudia tukio hili.”

Awali alikuwa na pambano la ndondi la mwaka 2022 lakini lilifutwa.

Hadi sasa mpinzani wake bado hajatangazwa, lakini inatarajiwa kuwepo kwa wapiganaji maarufu kutoka Ufaransa siku hiyo.

Hata hivyo, kupitia mitandao ya kijamii, Evra amemuita hadharani mchezaji wa zamani wa Liverpool, Suarez na kumtaka apande naye  ulingoni.

Kwa kejeli kuhusu tabia ya Suarez ya kung’ata, Evra alisema:

“Ninafanya mazoezi rasmi kwa ajili ya pambano langu la kwanza na wenye mamlaka ndio watachagua mpinzani wangu... waliniuliza nataka kupambana na nani. Nikasema: Luis Suárez. Nitagharimia pambano hilo kwa pesa zangu mwenyewe. Akiamua kuning’ata pia sawa tu.”

Evra na Suarez wana historia ndefu ya uhasama tangu walipokutana kwenye Ligi Kuu England na mshambuliaji huyo alihukumiwa na FA kwa kosa la ubaguzi wa rangi dhidi ya Evra wakati wa mechi kati ya Liverpool na Man United mwaka 2011.