Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Barcelona! Hili ni pigo

BARCA Pict

Muktasari:

  • Barcelona chini ya Hansi Flick imejengwa na idadi kubwa ya wachezaji vijana kutoka La Masia kama Pau Cubarsi, Alejandro Balde, Marc Casado, Gavi na Lamine Yamal, lakini wote wanadaiwa kwamba wanaweza kuondoka.

BARCELONA, HISPANIA: KUTOKANA na matatizo ya kifedha, ripoti zinaeleza Barcelona ipo katika hatari ya kupoteza wachezaji 10 kutoka kwenye akademi yao katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Barcelona chini ya Hansi Flick imejengwa na idadi kubwa ya wachezaji vijana kutoka La Masia kama Pau Cubarsi, Alejandro Balde, Marc Casado, Gavi na Lamine Yamal, lakini wote wanadaiwa kwamba wanaweza kuondoka.

Msimu huu, hadi sasa wababe hawa wamefanya vizuri katika La Liga, pia wamefika nusu fainali ya Copa del Rey na kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Ripoti zinadai kuchelewa kwa timu hii kurudi katika uwanja wao mpya wa Nou Camp kumesababisha hali ya uchumi wao kuyumba zaidi kutokana na kupungua kwa mapato ya uwanjani, hiyo imesababisha rais wa timu, Joan Laporta kufikia hatua ya kuuza haki za matangazo ya televisheni ya ndani ya timu hiyo ili kukusanya pesa.

Lakini Barca wanaendelea kukutana na matatizo hususani katika suala la usajili wa wachezaji kuelekea dirisha lijalo ambapo watatakiwa kuweka sawa ishu ya Dani Olmo inayetakiwa ilipe Pauni 50 milioni kwa ajili yake pia kusajili mastaa wengine.

Mkurugenzi wa La Liga awali alizuia Olmo na mshambuliaji mdogo Pau Victor wasisajiliwe hadi kiangazi kwa sababu Barcelona hawakuwa wanaruhusiwa na kanuni kuendelea kuwalipa mshahara.

Hata hivyo, baada ya sarakasi za hapa na pale, Barcelona walipata ruhusa kupitia baraza kuu la michezo la Hispania ambapo walipewa usajili wa muda, ikimaanisha kuwa wote wanaweza kucheza hadi Aprili 7. Kwa mujibu wa gazeti la Catalan Sport, Barca huenda ikalazimika kuachana na wachezaji kumi ambao watakuwa ni katika orodha ya vijana wao wenye umri chini ya miaka 19 ifikapo mwisho wa msimu huu.

Idadi ya wachezaji hawa vijana mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na kama mambo ya kiuchumi hayatokuwa mazuri, wataondoka wakiwa huru.

Jambo jingine linaloonekana kuwa litachangia zaidi kwa mastaa hao kuondoka ni mpango wa Barca wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Newcastle, Alexander Isak ambaye wanahitaji aende kuziba pengo la Robert Lewandowski ambaye umri umeshamtupa mkono.