Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maresca ajiondoa kwa Palmer

Muktasari:

  • Palmer alianza msimu huu vizuri lakini kwa sasa amekumbwa na kipindi kigumu, hajafunga bao katika mechi 16 zilizopita za Chelsea, hali ambayo imemfanya apokee maneno makali kutoka kwa mashabiki kwani hakuwahi kuwa katika kiwango kibovu kama hiki tangu ajiunge na Chelsea mwaka 2023, kwa Pauni 40 milioni akitokea Manchester City.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca amesema hahusiki na kushuka kwa kiwango cha staa wa timu hiyo, Cole Palmer na amesisitiza huenda ana presha.

Palmer alianza msimu huu vizuri lakini kwa sasa amekumbwa na kipindi kigumu, hajafunga bao katika mechi 16 zilizopita za Chelsea, hali ambayo imemfanya apokee maneno makali kutoka kwa mashabiki kwani hakuwahi kuwa katika kiwango kibovu kama hiki tangu ajiunge na Chelsea mwaka 2023, kwa Pauni 40 milioni akitokea Manchester City.

Maresca amekanusha madai ya kwamba mfumo wa Chelsea ndio sababu ya matatizo ya Palmer. Akizungumza kabla ya mechi dhidi ya Everton, kocha huyo wa Kiitaliano alisisitiza staa huyo ameshuka kiwango kutokana kwa sababu za kiakili zaidi kuliko kiufundi.

“Kwa hakika, ni kiakili. Sidhani kama ni kwa sababu ya mbinu au uwezo wa kiufundi, kwa sababu Cole bado ni yule yule aliyefunga mabao msimu huu akiwa nasi. mfumo tunaocheza ni ule ule, kocha ni yule yule. timu ni ile ile. Hakuna kilichobadilika kumhusu Cole, wala Cole mwenyewe hajabadilika. Ni suala la kiakili kwa sasa. Bila shaka, unaweza kuona kuwa ana presha kidogo kwa sababu anataka kusaidia timu.”

Tangu kuanza kwa msimu huu Palmer amecheza mechi 39 za michuano yote, amefunga mabao 14 na kutoa asisti tisa.