Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi apata dili nono Wydad AC

NABI Pict

Muktasari:

  • Taarifa hizo zinaeleza kuwa bonasi hizo zitahusishwa na nafasi ambayo Wydad itamaliza katika Ligi Kuu ya Morocco, Botola Pro, hususan kumaliza katika nafasi mbili za juu.

CASABLANCA, MOROCCO: ALIYEKUWA kocha wa Yanga na Kaizer Chiefs, Nasreddine Nabi, atalipwa dola 368,000 za Marekani kwa mwaka katika kibarua chake kipya ndani ya Wydad Casablanca.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Morocco, ikiwamo LesiteInfo, Nabi atapokea kiasi hicho cha fedha ni mshahara wake tu hakijumuishi bonasi zinazoweza kulipwa kutokana na matokeo ya timu.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa bonasi hizo zitahusishwa na nafasi ambayo Wydad itamaliza katika Ligi Kuu ya Morocco, Botola Pro, hususan kumaliza katika nafasi mbili za juu.

Lengo la klabu hiyo ni kumaliza katika nafasi zitakazoipa tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, hivyo mafanikio ya Nabi yatapimwa pia kwa uwezo wake wa kuifikisha timu katika malengo hayo.

Katika kulifikia hilo Nabi aliiongoza Wydad Casablanca kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Union Touarga katika mchezo wake wa kwanza tangu kutangazwa kuwa kocha wa timu hiyo.

Kocha huyo raia wa Tunisia alitangazwa rasmi kuwa kocha wa Wydad Ijumaa, baada ya kuwa hana timu tangu alipoachana na wapinzani wao wa jiji hilo, Raja Casablanca, Septemba mwaka huu.

Katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa wiki, Aymane El Hassouni ndiye aliyeamua matokeo baada ya kufunga bao pekee kwa mkwaju wa penalti, akiipa Wydad ushindi muhimu katika mwanzo wchini ya Nabi.

Mbali na kuanza kwa ushindi, Nabi pia anatajwa kuwa amesaini mkataba utakaomuweka Wydad hadi mwisho wa msimu wa 2026/27.