Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Owen ataja warithi wa Mo Salah, Nunez

Muktasari:

  • Salah mkataba wake utafika tamati mwishoni mwa msimu huu, wakati Nunez amekuwa akihusishwa na mpango wa kutimkia Saudi Pro League.

LIVERPOOL, ENGLAND: STRAIKA wa zamani wa Liverpool, Michael Owen amewataka mabosi wa timu hiyo kuangalia ndani ya klabu za Ligi Kuu England katika msako wao wa kupata wachezaji wa kuja kuchukua mikoba ya Mohamed Salah na Darwin Nunez.

Salah mkataba wake utafika tamati mwishoni mwa msimu huu, wakati Nunez amekuwa akihusishwa na mpango wa kutimkia Saudi Pro League.

Wachezaji ambao Owen anaamini wanaweza kuja kuwabadili Mo Salah na Nunez ni straika wa Newcastle United, Alexander Isak na yule mkali wa Bournemouth, Antoine Semenyo.

Isak alishawahi kuelezewa huko nyuma kuwapo kwenye rada ya Liverpool, wakati Semenyo amekuwa kwenye kiwango bora kabisa Bournemouth, kitu kinachomfanya awindwe na timu nyingi.

Mghana huyo aliyezaliwa London, Semenyo, 25, amefunga mabao tisa na asisti tano katika michuano yote aliyocheza msimu huu. Hicho ni kiwango bora kabisa katika maisha yake ya soka, akiwa amejiunga na timu yake ya sasa akitokea Bristol City, Januari 2023.

Isak, amekuwa na kiwango bora kabisa msimu huu. Mkali huyo wa kimataifa wa Sweden amefunga mabao 23 katika michuano yote. Staa huyo wa Newcastle amefunga mara nne pia kwenye mechi nne za UEFA Nations League.

"Kumekuwa na uvumi wa wachezaji tofauti kwa siku za karibuni," alisema Owen.

"Alexander Isak, bila shaka amekuwa akifunga mabao Newcastle, hivyo itakuwa usajili mzuri kama Liverpool itampata, lakini nina uhakika kuna timu nyingine zinamtaka na Newcastle haitataka kumpoteza.

"Nampenda Antoine Semenyo huko Bournemouth, ambaye amekuwa akicheza nafasi sawa na Salah. Nampenda, ni kijana, lakini ana nguvu sana, anafunga na ni mchezaji mzuri. Kwa kusema hivyo, sina maana anaweza kumbadili Mo Salah.

Wakati Owen akiwataka Isak na Semenyo watue Liverpool, staa mwenzake wa zamani wa England, Alan Shearer amekuwa na mawazo tofauti, akimtaka Liam Delap wa Ipswich Town."