Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri ya Amorim kumtaka Cunha yafichuka

Muktasari:

  • Inaelezwa kuwa kocha wa Manchester United, Ruben Amorim amevutiwa na kiwango cha mchezaji huyo anachoendelea kukionyesha.

Manchester United inaamini mshambuliaji wa Wolverhampton, Matheus Cunha, ndiye chaguo sahihi la kuimarisha safu yao ya ushambuliaji msimu ujao, kufuatia upungufu wa mabao ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na kocha, Ruben Amorim.

Man United hadi sasa imecheza michezo 33 ya Ligi Kuu England ambapo imefunga mabao 38 huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara 46 ikiwa ni rekodi mbaya kwa timu hiyo inayoshika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi.

Kocha wa United, Ruben Amorim amesema safu yake ya ushambuliaji haifungi mabao ya kutosha jambo linaloifanya timu hiyo kukosa idadi kubwa ya mabao kwenye Ligi Kuu msimu huu.

"Ni jukumu la timu nzima kufunga mabao. Hatufungi ya kutosha na hilo ni tatizo katika Ligi hii," amesema Amorim.

Mpaka sasa Matheus Cunha ndiye chaguo la kwanza kwa United akionekana kumvutia zaidi Ruben Amorim kutokana na mwendelezo mzuri wa kiwango anachoendelea kukionyesha msimu huu.

Mbrazili huyo amecheza jumla ya michezo 28 ya Ligi Kuu England akihusika katika mabao 18 baada ya kufunga 14 na kutoa asisti nne ndani ya kikosi cha Wolverhampton.

Kwa mujibu wa Jarida la Daily Mail, wakala wa mchezaji huyo ameshazungumza na Man United huku dau la kumchomoa kwenye viunga vya Wolverhampton likitajwa kuwa ni dola za Marekani 77.5 milioni.

Mbali na Cunha, washambuliaji wengine wanaohusishwa kuwindwa na United ni Victor Osimhen anayecheza Galatasaray kwa mkopo akitokea Napoli, Viktor Gyökeres (Sporting Lisbon), Liam Delap (Ipswich Town) na Benjamin Šeško (RB Leipzig).

United inatakiwa kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi chake msimu ujao ikiwemo kwa kusajili wachezaji bora zaidi kutokana na mwendelezo mbaya waliouonesha msimu huu