Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TAJIRI ANAUMIA: Mmiliki wa zamani ana jambo Chelsea

Muktasari:

  • Abramovic ambaye aliiongoza klabu hiyo hadi kipindi cha mafanikio makubwa zaidi katika historia yake, hivi karibuni alizungumza kuelekea kuzindua kitabu chake yakiwa ni mahojiano yake ya kwanza tangu mwaka 2021 alipohojiwa na jarida la Forbes.

LONDON, ENGLAND: TAJIRI na mmiliki wa zamani wa Chelsea, Roman Abramovich anadaiwa kuwa bado roho inamuuma juu ya kuiuza timu hiyo ambayo kwake ilikuwa ni sehemu ya furaha yake.

Abramovic ambaye aliiongoza klabu hiyo hadi kipindi cha mafanikio makubwa zaidi katika historia yake, hivi karibuni alizungumza kuelekea kuzindua kitabu chake yakiwa ni mahojiano yake ya kwanza tangu mwaka 2021 alipohojiwa na jarida la Forbes.

Abramovich anazidi kudhibitiwa kwa vikwazo na serikali ya Uingereza kutokana na madai ya uhusiano wake wa karibu na rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Alianza kupewa vikwazo hivyo chini ya serikali ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Boris Johnson baada ya kuzuka kwa mgogoro kati ya Russia na Ukraine mwaka 2022.

Mali za tajiri huyo mwenye umri wa miaka 58 zilizuiwa na alilazimika kuiuza Chelsea ambayo hakuruhusiwa kuendelea kuimiliki. Mchakato wa kuiuza timu ulikamilika Machi 2022 pale kampuni ya Todd Boehly-Clearlake Capital iliponunua hisa zote.

Mahojiano ya tajiri huyo yameandikwa katika kitabu cha ‘The Inside Story of the Sale of Chelsea FC’ kilichoandikwa na Nick Purewall ambacho kinatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Mbali ya mahojiano katika kitabu hicho mchezaji wa zamani wa Chelsea,  John Obi Mikel ambaye alikuwa miongoni mwa vipenzi vya Abramovich alisema mara kadhaa ambazo amekuwa akizungumza na tajiri huyo huonyesha hasira juu ya kulazimishwa kuiuza Chlsea.

“Kilichotokea ni bahati mbaya alipoteza klabu ya soka. Bado nazungumza na watu wake wa karibu na yeye mwenyewe. Kiukweli bado inamuumiza. Anasikitishwa kuhusiana na kilichotokea,” alisema Obi.

“Hafurahii kuona kwamba alipoteza ‘mtoto wake’ kwa sababu Chelsea Football Club ilikuwa ni timu aliyoipenda. Alijali sana kuhusu klabu hiyo na alipenda kila kitu kuanzia wachezaji na mashabiki.”

Uongozi wa Abramovich wa miaka 19 ulianza 2003 ambapo chini yake Chelsea ilishinda makombe 21 ikiwemo matano ya Ligi Kuu England, matano ya FA na mawili Ligi ya Mabingwa ilhali mawili yakiwa ya Europa League.