Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WAMOTO! Lazio, Dortmund mdogomdogo

WAMOTO Pict

Muktasari:

  • Timu ya Lazio ina pointi 22 baada ya kucheza mechi nane msimu huu sawa mabingwa watetezi, Inter Milan, ambao wanaongoza msimamo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakiwa na alama kama za lazio.

MILAN, ITALIA: LAZIO ilipanda hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Italia (Serie A) kwa muda, baada ya kuichapa Parma mabao 2-1 nyumbani, huku Roma ikitoka sare ya mabao 3-3 na Napoli katika mchezo wa kusisimua uliofanyika jijini Naples baada ya kusawazisha mara mbili.

Timu ya Lazio ina pointi 22 baada ya kucheza mechi nane msimu huu sawa mabingwa watetezi, Inter Milan, ambao wanaongoza msimamo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakiwa na alama kama za lazio.

Lazio ilipata bao la kwanza dakika ya 50 kupitia Kenneth Taylor, aliyefunga bao lake la kwanza msimu huu, kabla ya Diego Carlos wa Parma kujifunga wakati akijaribu kuzuia krosi. Parma ilipata bao la kufutia machozi mwishoni mwa mchezo kupitia Simone Lontani.

Roma, inayoshika nafasi ya tatu, ilijikuta nyuma kwa mabao 2-0 na baadaye 3-2 katika dakika za mwisho, hivyo ikafurahia kupata pointi moja jijini Naples. Sare hiyo iliendeleza rekodi yake ya kutopoteza mechi za ligi kwa michezo 15 mfululizo, rekodi iliyoanzia Aprili.

Frank Anguissa aliipa Napoli bao la kuongoza kwa shuti la kuvutia la juu akiwa hewani (overhead kick), kabla ya Scott McTominay kuongeza bao la pili. Wakati huo, Napoli ilionekana kuwa na udhibiti kamili wa mchezo, lakini mabao mawili ndani ya dakika nne kutoka kwa Matías Soulé na Leonardo Balerdi yaliirudisha Roma mchezoni na kusawazisha matokeo.

WAMO 01

McTominay alipofunga bao lake la pili katika dakika za mwisho, kasi ya mchezo ilionekana kuhamia upande wa Napoli. Hata hivyo, Balerdi aliifungia Roma bao la kusawazisha kwa kichwa zikiwa zimesalia dakika moja kabla ya mchezo kumalizika.

Como iliendeleza kiwango chake bora baada ya Anastasios Douvikas kuifungia mabao mawili ndani ya dakika 11 na kuipa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sassuolo. Matokeo hayo yaliipandisha Como hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.


DORTMUND, BAYERN KAZINI KUNA KAZI

Nchini Ujerumani, Maximilian Beier alifunga bao dakika ya 80 na kuiwezesha Borussia Dortmund kupanda hadi kileleni mwa Bundesliga kwa muda baada ya ushindi mgumu wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Katika mchezo ambao nafasi nyingi za wazi hazikupatikana, Jobe Bellingham aliingia akitokea benchi na kutoa pasi nzuri iliyomfikia Beier, ambaye pia alikuwa ameingia akitokea benchi, kisha kufunga chini ya dakika moja.

Ushindi huo mwembamba ulikuwa wa kwanza kwa Dortmund katika ligi tangu katikati ya Septemba na uliifanya timu hiyo kupaa hadi kileleni kwa muda kabla ya Bayern Munich kuishusha baaye ilipoishinda Freiburg kwa mabao 3-1. Dortmund na Bayern zote zina pointi sawa 17 zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Niclas Fullkrug aliendeleza rekodi ya kufunga katika mechi sita mfululizo za Bundesliga, wakati Werder Bremen ilipoishinda Mainz mabao 3-2 ugenini. Fullkrug, aliyerejea Bremen kwa mkopo akitokea West Ham katika dirisha la usajili la majira ya joto, alifunga penalti mbili ndani ya dakika 25 za mwanzo wa mchezo. Ludovit Reis alifunga bao jingine la Bremen, huku Anthony Caci na Lee Jae-sung wakiifungia Mainz.

WAMO 02

RB Leipzig ilipata ushindi rahisi wa mabao 4-0 nyumbani dhidi ya Elversberg, iliyopanda daraja msimu huu.

Rayan Philippe wa Paderborn alifunga dakika ya 88 dhidi ya Hamburg, klabu ambayo bado inamiliki mkataba wake, na kuipa timu hiyo iliyopanda daraja ushindi wa bao 1-0.

Augsburg na Union Berlin zilitoka sare ya bao 1-1, huku kila timu ikimaliza mchezo ikiwa na wachezaji 10 baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu.

Cologne na Schalke zilitoka sare tasa katika mchezo uliogubikwa na tukio la kugongana vichwa kati ya Robin Gosens wa Schalke na Soufiane El-Faouzi wa Cologne. Wachezaji hao walilazimika kuondolewa uwanjani katika kipindi cha kwanza.


WAMO 03

ATLETICO KAMA KAWA

Achana na matokeo ya El Clasico katika Real Madrid na Barcelona, lakini katika Ligi Kuu Hispania (La Liga), Atletico Madrid iliendeleza presha kwa timu zilizo juu baada ya kuichapa Deportivo Coruaa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Riyadh Air Metropolitano.

Wakati huo huo, Georges Mikautadze aliifungia Villarreal bao la ushindi katika dakika za nyongeza na kuipa timu yake ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Valencia katika mchezo wa watani wa jadi.

Valencia ilimaliza mchezo ikiwa na wachezaji 10 baada ya Harvey Elliott kutolewa kwa kadi nyekundu, huku timu zote zikimaliza mchezo zikiwa na wachezaji pungufu.


LENS WANAKIMBIZA POLEPOLE

Nchini Ufaransa, Lens ilitoka nyuma na kuichapa Paris FC mabao 2-1, huku Thorgan Hazard akifunga bao la ushindi dakika ya 83 na kuisogeza timu yake hadi pointi tatu nyuma ya vinara wa Ligue 1.

Lens, iliyomaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita, ilianza msimu huu kwa kusuasua. Hata hivyo, imeshinda mechi mbili mfululizo za ligi ya Ufaransa na kufikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi nane.