Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TMK Family bado kidogo tu!

TMK Pict

Muktasari:

  • Temba ameliambia Mwanaspoti Kundi la TMK Wanaume litarudi na kuanza kazi ya muziki kama lilivyokuwa zamani na bado mambo madogo tu kufanikisha hilo.

BAADA ya mmoja wa memba wa TMK Wanaume Family, Mheshimiwa Temba kuonekana kufanya kazi na Sir Juma Nature mnamo Mei mwaka huu kupitia ngoma iitwayo ‘Warembo’, kuna watu waliamini ule mzuka wa TMK unarejea upya, lakini mambo yapo tofauti.

Temba ameliambia Mwanaspoti Kundi la TMK Wanaume litarudi na kuanza kazi ya muziki kama lilivyokuwa zamani na bado mambo madogo tu kufanikisha hilo.

Kuthibitisha hilo, Temba alisema anatarajia kuandaa kolabo moja matata mwaka huu wa 2025 ili kurudisha rasmi kundi hilo.

Alisema wanatarajia ujio wao huo kuwa wa tofauti kwa kubadilisha mfumo wa utendaji wa kazi kutoka wimbo kuwa na dakika tano na kuwa dakika tatu.

“TMK Wanaume Family bado lipo, kukaa kimya siyo sababu ya kundi kuonekana kuvunjika na ndiyo maana hata unaona ikipatikana shoo tunaenda kupiga kama timu, hivyo ni mfumo tu wa utendaji huwa unasababisha kuwa kimya,” alisema Mhe Temba ambaye ni mmoja ya waliolinogesha kundi hilo enzi hizo sambamba na Nature, KR Mulla, Chegge na wengine kabla ya kusambaratika. Mhe Temba aliongeza, pamoja na ukimya wa kutoa wimbo, bado ana sauti yake ileile ambayo huilinda isipotezee.

Kundi la TMK Wanaume lilikuwa likiundwa na mastaa kibao wakiwemo Temba, Juma Nature, Y Dash, Chegge, Inspector Haroun, Dolo, Rich One na KR.