Utamu Kolabo ya Mr Eazi, Moliy katika Comfort
Muktasari:
- Ngoma hii yenye mahadhi ha Afropop, amemshirikisha mwanamuziki kutoka Ghana, Moliy anayefahamika kujitengenezea umalkia wake kwenye kibao 'Shake it To The Max' (Done With Ya Ex).
STAA wa muziki wa Afropop, Mr Eazi, hajawatelekeza mashabiki zake, kwani amerudi na wimbo mpya uitwao Comfort.
Ngoma hii yenye mahadhi ha Afropop, amemshirikisha mwanamuziki kutoka Ghana, Moliy anayefahamika kujitengenezea umalkia wake kwenye kibao 'Shake it To The Max' (Done With Ya Ex).
Comfort una mchanganyiko wa sauti ya kipekee kutoka kwa Mr Eazi ya Banku Music na sauti tamu ya Moliy, ukiupatia wimbo huo hisia tamu na ya kufurahisha.
Kazi hiyo imepitia kwenye mikono iliyobarikiwa ya Ragee, mtayarishaji maarufu wa Nigeria nyuma ya hit za hivi karibuni za Davido (Unavailable) na Ayra Starr (Hot Body, Who's Dat Girl.
Comfort imechanganya Afrobeats, Dancehall na R&B kwa mdundo wa kustarehesha na melodi inayobamba, ukiwapa Mr Eazi na Moliy nafasi ya kuonesha vipaji vyao huku wakileta nguvu ya kustarehe na mahaba kwenye wimbo huo.
Akizungumzia wimbo huo, Mr Eazi amesema: "Hili ni toleo lililoboreshwa la sauti yangu ya kipekee. Ninatengeneza muziki wa kina dada, muziki mtamu, mwepesi, unaowasifia kina dada. Ni kuhusu kuweka mambo mepesi, ya kufurahisha na yanayokufanya ujisikie vizuri, huku bado nikiwapa watu sauti ile ile ya Mr Eazi wanayoijua na kuipenda."
Ngoma hiyo imekuja katika kipindi cha mafanikio ya muziki mpya kutoka kwa Mr Eazi mwaka 2026.
Mapema mwaka huu, Mr Eazi, aliungana na mtayarishaji wa Dancehall wa Marekani, Dre Skull kwa mfululizo wa nyimbo zikiwemo "Lambo" akiwa na Vybz Kartel, "Hide Your Love" na "Remember That," akiwa na gwiji wa dancehall Cham.