Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asante Morocco, hatukudai chochote

MOROCCO Pict

Muktasari:

  • Hapa kijiweni tunamshukuru kwa mchango na kujitolea kwake kwa taifa na tunamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya siku za usoni.

HAIKUWA habari ya kushangaza juzi pale TFF ilipotangaza kusitisha mkataba wa Kocha Hemed Suleiman 'Morocco' kuinoa timu ya taifa, Taifa Stars.

Kwa sisi hapa kijiweni tuliolizoea soka letu tunaona ni kawaida maana huwa siyo rahisi kocha kuvumiliwa, huku akiwa hajapata matokeo mazuri kwa mechi nyingi mfululizo.

Morocco hakuwa amepata ushindi katika mechi sita na tano ni za mashindano na nyingine moja ya kirafiki, kwani timu hiyo ilitoka sare mbili tu huku ikipoteza michezo minne.

Mechi za mashindano alizotoka sare ni dhidi ya Afrika ya Kati na Congo na alizopoteza ni mbele ya timu za Morocco, Niger na Zambia na nyingine moja Taifa Stars ilifungwa ya kirafiki dhidi ya Iran.

Lakini pamoja na yote, hatupaswi kumdai chochote Hemed Morocco kwani kwa nafasi na uwezo wake amejitahidi sana katika kipindi ambacho amesimamia benchi la ufundi la Taifa Stars ingawa mwisho wake haujawa mzuri kwa hayo matokeo.

Morocco ametuwezesha kufuzu Fainali za AFCON mwaka huu, huku akiwa na kundi kubwa la wachezaji wanaocheza soka katika klabu za hapa nchini, pia katika Fainali za CHAN Stars iliingia hatua ya robo fainali ambayo haikuwahi kufika.

Ameachana na Taifa Stars akiwa ameipa mafanikio makubwa ambayo kwa sisi hapa kijiweni hatudhani kama kuna kicha yeyote mzawa amewahi kuyapata akiwa anainoa timu hiyo tangu ilipoanza kushiriki mashindano ya kimataifa.

Kama ilivyo kawaida, hakuna mwanzo usio na mwisho ndivyo imetokea kwa Morocco kwani asingeweza kubaki pale milele, ilikuwa lazima siku moja angeondoka na kumpisha mwingine.

Hapa kijiweni tunamshukuru kwa mchango na kujitolea kwake kwa taifa na tunamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya siku za usoni.