Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwaheri Pantev hutakiwi kuwajibika mwenyewe

PANTEV Pict

Muktasari:

  • Kijiwe kilitegemea kuwa Pantev angeondoka Simba siku moja, lakini hakikudhani kwamba uamuzi wa kumuondoa raia huyo wa Bulgaria ungekuwa wa haraka kiasi hiki kwa vile alikuwa bado hajafikisha angalau muda wa miezi mitatu ambayo inatosha kuingiza falsafa na mbinu zake.

KIBARUA cha Meneja Mkuu wa Simba, Dimitar Pantev kiliota nyasi rasmi siku ya Jumanne, Desemba 2, 2025 nyakati za jioni baada ya Simba kutangaza kuachana naye.

Kijiwe kilitegemea kuwa Pantev angeondoka Simba siku moja, lakini hakikudhani kwamba uamuzi wa kumuondoa raia huyo wa Bulgaria ungekuwa wa haraka kiasi hiki kwa vile alikuwa bado hajafikisha angalau muda wa miezi mitatu ambayo inatosha kuingiza falsafa na mbinu zake.

Lakini ndio hivyo, uongozi wa Simba umeamua kuachana naye na hilo linaonekana kuchangiwa zaidi na matokeo ambayo timu hiyo imepata katika mechi mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro Luanda na Stade Malien.

Kabla hata ya kupoteza kwa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Petro na kisha ikafungwa mabao 2-1 na Stade Malien ugenini, Simba ilishaanza kuonyesha dalili za kupoteza imani kwa Pantev hasa baada ya timu hiyo kutoka sare tasa na Nsingizini kwenye mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya mashindano hayo.

Hata hivyo, hapa kijiweni tunaamini kwamba Pantev alikuwa ni sehemu ndogo tu ya kilichoiangusha Simba katika mechi hizo mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Iko wazi kwamba kilichoigharimu Simba ni kukosekana kwa utulivu na maelewano baina ya viongozi wa timu hiyo katika kipindi cha kabla na wakati wa mechi hizo.

Na hilo limethibitishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu hiyo ambaye alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akisema kuwa kuna watu ndani ya timu hiyo wanafurahia kuona ikipoteza mchezo.

Sasa kama viongozi wenyewe hawapatani hadi inafikia hatua mmoja wao anazungumza hadharani katika vyombo vya habari, ni vigumu kwa timu kujiandaa vizuri na michezo husika.

Mafanikio ya timu hayaletwi na benchi la ufundi pekee. Kama viongozi hawako sawa, ni vigumu timu kufanikiwa.