Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba wasifanye kosa la Mwalimu kwa Libasse

LIBASE Pict

Muktasari:

  • Maana yule Mwalimu walikuwa na uwezekano mkubwa wa kubaki naye kikosini, lakini kujisikilizia kwao kukawaponza jamaa akachukuliwa Yanga kibabe.

LILE kosa la kuchelewa chelewa ambalo Simba walilifanya katika kukamilisha usajili wa Selemani Mwalimu hadi akatimkia Yanga, wasithubutu kulifanya kwa Libasse Gueye.

Maana yule Mwalimu walikuwa na uwezekano mkubwa wa kubaki naye kikosini, lakini kujisikilizia kwao kukawaponza jamaa akachukuliwa Yanga kibabe.

Sasa mwishoni mwa msimu huu, mkali wao Libasse Gueye atakuwa anamaliza mkataba hivyo atakuwa huru kujiunga na timu yoyote ile ama kubaki Simba na mzigo wote atachukua yeye.

Mbaya zaidi mwezi wa kwanza tu mwakani ataruhusiwa kufanya makubaliano ya kujiunga na timu nyingine kwa vile mkataba wake utakuwa umebakiza muda wa miezi sita.

Maana Yanga usikute muda huu wanajipanga kikamilifu kuwapa pigo tena kama ambavyo walifanya katika madirisha yaliyopita ya usajili ambayo walichukua wachezaji wao vipenzi na kuwaumiza mashabiki wa Simba.

Na ukiangalia kwa sasa mchezaji wa moto zaidi pale katika kikosi cha Simba ni Libasse Gueye maana kiwango na namba zake uwanjani vinaongea vyenyewe bila hata sisi kuongeza kitu.

Wakati tupo hapa kijiweni juzi tukamsikia yule bosi mkubwa wa Yanga akitamba katika redio moja hivi tena akiapia kwa kulitaja jina la Mungu kuwa kuna watu wajiandae kwa kuuana.

Yaani kwa tafsiri ya haraka haraka ni kwamba atachukua wachezaji au mchezaji wao muhimu katika hilo dirisha dogo hivyo itapelekea watakaoporwa wagombane juu ya hao wachezaji au huyo mchezaji.

Haya kazi kwao Simba kuhusu Gueye wakizubaa yasije yakawakuta tena yale yaliyotokea kwa Selemani.