Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viberenge: Mastaa waliotikisa EPL kwa spidi msimu huu

VIBORENGE Pict

Muktasari:

  • Barcola, mwenye miaka 24, alijiunga na Liverpool mwezi Agosti kwa ada ya Pauni 123 milioni akitokea PSG ambako pamoja na kutwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1), pia alikuwa akijulikana kwa kasi yake kubwa.

LONDON, ENGLAND: WINGA wa mpya wa Liverpool, Bradley Barcola amerekodiwa kuwa mchezaji mwenye kasi zaidi katika Ligi Kuu England baada ya michezo mitano akiongoza orodha ya 20 bora ya wachezaji wenye kasi kubwa hadi sasa.

Barcola, mwenye miaka 24, alijiunga na Liverpool mwezi Agosti kwa ada ya Pauni 123 milioni akitokea PSG ambako pamoja na kutwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1), pia alikuwa akijulikana kwa kasi yake kubwa.

Katika viwango vipya vya kasi ya juu vilivyowekwa na FotMob, nyota huyo ametawazwa kuwa mfalme wa wachezaji wenye kasi baada ya kufikia kasi ya kilomita 35.9 kwa saa.

VIBE 01

Mchezaji alifikia kasi hiyo wakati wa mchezo wake wa kwanza akiwa na Liverpool dhidi ya Ipswich Town, ambao timu yake ilishinda mabao 2-0 mwanzoni mwa mwezi uliopita, baada ya wachezaji wa timu hiyo pinzani kumpa nafasi kubwa ya kukimbia na kuonyesha kasi yake.

Hata hivyo, katika mechi zake mbili zilizofuata; zote akiwa kwenye kikosi cha kwanza ameshindwa kufikia kasi hiyo tena, huku pia akipata ugumu wa kuanza kufunga mabao.

Kwa upande mwingine wa viwango hivyo, mchezaji wa uwanjani mwenye kasi ndogo zaidi katika ligi hiyo ni beki wa Tottenham Hotspur, Tosin Adarabioyo, ambapo mikoba huyo wa kati aliyejiunga na Spurs akitokea Chelsea katika dirisha la usajili lililopita amerekodi kasi ya juu isiyozidi kilomita 21.4 kwa saa.

Akirejea kileleni mwa orodha, Barcola ambaye bado hajafunga bao wala kutoa asisti kwa Liverpool amempiku Bryan Mbeumo wa Manchester United na kuchukua nafasi ya kwanza. Winga huyo wa United alikosa kwa tofauti ndogo sana, baada ya kurekodi kasi ya kilomita 35.4 kwa saa.

VIBE 02

Nyuma ya Mbeumo kuna mastaa waliofungana wanne wanaoshika nafasi ya tatu, ambapo nyota hao wenye kasi walirekodi kiwango kilichokuwa chini kidogo ya cha Mkameruni huyo. Gonzalo Garcia wa Fulham; beki wa pembeni wa Coventry City, Milan van Ewijk; Pedro Neto wa Chelsea na Robinio Vaz wa Hull City wote walirekodi kasi ya juu ya kilomita 35.3 kwa saa.

Aliyefuatia kwa kasi kidogo chini yao ni winga wa Newcastle United, Jacob Murphy, ambaye licha ya kuwa na nafasi ndogo katika kikosi cha sasa cha Magpies chini ya kocha Matthias Jaissle amefikia kasi ya kilomita 35.2 kwa saa.

Nyota wa Kibrazili anayekipiga Bournemouth, Rayan, amesifiwa kwa msimu wake wa kwanza katika soka la England, akiwatesa mabeki kutoka upande wa kulia na kwa sehemu kubwa ya mchezo wa winga huyo ni kasi yake pembeni mwa uwanja, na alirekodi kasi iliyokuwa chini kidogo ya Murphy akitumia kilomita 35.1 kwa saa.

VIBE 03

Jambo mojawapo la kushangaza ni kwamba Anthony Elanga, ambaye wengi humtaja kuwa miongoni mwa nyota wenye kasi zaidi barani Ulaya, anashika nafasi ya 12, licha ya kuanza msimu kwa kasi kabla ya kuumia. Kasi yake ya kilomita 34.9 kwa saa iko chini kwa kiasi kikubwa ya kasi yake ya juu ya kilomita 36.35 kwa saa aliyorekodi msimu uliopita, ambayo ingemuweka kileleni mwa orodha hii.

Straika Alexander Isak amekosolewa kwa kuonekana kupoteza sehemu ya kasi yake tangu alipohamia Liverpool kwa rekodi ya Pauni 125 milioni msimu uliopita, lakini ameingia kwenye 20 bora akiwa nafasi ya 14, akiwa na kasi ya juu ya kilomita  34.76 kwa saa ikiwa chini kwa kilomita 0.16 tu ya aliyekuwa nyota mwenzake kikosini, Elanga.

Hata hivyo, jambo ambalo anaonekana kulirejesha msimu huu ni uwezo wake wa kumalizia nafasi. Mswedeni huyo ameanza msimu wake kwa kiwango bora zaidi kuwahi kuwa nacho katika Ligi Kuu England akifunga mabao manne katika mechi tano likiwamo la ushindi dhidi ya Bournemouth.

VIBE 04

Mpinzani wake katika mbio za kiatu cha dhahabu (Golden Boot), Erling Haaland, anajulikana kwa kasi yake ya kutisha, lakini ameingia kwenye 20 bora kwa tofauti ndogo kupitia kufungana na wachezaji sita wanaoshika nafasi ya 19, ambapo mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Norway amerekodi kasi ya juu ya kilomita 34.6 kwa saa, sawa na Antonee Robinson wa Fulham, Mohamed Belloumi wa Hull City, usajili mpya wa Liverpool Jeremy Jacquet, beki wa Chelsea Josh Acheampong na mwisho straika wa Leeds United, Dominic Calvert-Lewin.

VIBE 05

Lakini, jambo ambalo Haaland hawezi kulinganishwa nalo ni uwezo wake wa kufunga mabao, kwani kwa mara nyingine anaongoza chati ya wafungaji mbele ya Isak. Mchezaji huyo wa Manchester City amefunga mabao matano katika mechi tano, na kwa kufanya hivyo ameisaidia timu kukaa kileleni mwa msimamo wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa, ikiwa na rekodi ya kushinda kwa asilimia 100.