Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam, Simba zinarudi mzigoni Ligi Kuu

LIGI KUU Pict

Muktasari:

  • Katika mechi nyingine, Azam FC, iliyofuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya pili mfululizo, itakutana na Mbeya City ikiwa na lengo la kupata ushindi utakaoiweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa.

LIGI Kuu Bara inaendelea tena, huku vinara wa ligi hiyo, Simba wakiingia dimbani dhidi ya Fountain Gate wakitafuta pointi tatu muhimu zitakazowawezesha kuendeleza ubabe wao na kuimarisha nafasi yao kileleni mwa msimamo.

Katika mechi nyingine, Azam FC, iliyofuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya pili mfululizo, itakutana na Mbeya City ikiwa na lengo la kupata ushindi utakaoiweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa.

Wakati huohuo, Coastal Union na Kagera Sugar zitachuana zikitafuta matokeo mazuri yatakayozisaidia kujiimarisha baada ya kufanya vibaya michezo iliyopita.

Simba inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 24 baada ya kushinda michezo yote minane iliyocheza. Inafuatwa na Yanga yenye pointi 19, huku Azam FC ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 17.


LIGI 02

FOUNTAIN GATE VS SIMBA

Simba itashuka dimbani kukutana na Fountain Gate katika mchezo unaoipa nafasi ya kuendeleza mwenendo wake mzuri. Hata hivyo, italazimika kuvunja upinzani wa Fountain Gate, itakayokuwa ikicheza nyumbani katika Uwanja wa Kwaraa, Babati.

Rekodi za hivi karibuni zinaipa Simba nafasi nzuri ya kujiamini dhidi ya Fountain Gate. Katika mchezo wao wa mwisho wa ligi, uliofanyika Aprili 15, 2026, Simba ilipata ushindi wa mabao 3-0 ugenini. Kabla ya hapo, Septemba 25, 2025, iliifunga Fountain Gate kwa mabao 3-0 nyumbani.

Matokeo hayo yanaonyesha katika michezo hiyo miwili ya ligi, Simba imefunga mabao sita bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa. Kwa upande mwingine, Fountain Gate italenga kuzuia matokeo kama hayo yasijirudie, hasa ikitumia faida ya kucheza mbele ya mashabiki wake.

Katika msimu huu, Fountain Gate imekuwa na matokeo yasiyoridhisha. Katika michezo minane iliyocheza, imeshinda mmoja, imetoka sare mara mbili na kupoteza mitano, hivyo kujikusanyia pointi tano.

Akizungumzia mchezo huo, kocha wa Simba, Steve Barker, amesema: “Tunajua mechi itakuwa ngumu kwa sababu msimu uliopita tulitoka sare ya 1-1 kwenye uwanja huohuo. Hivyo, tunaingia katika mchezo huu kwa tahadhari kubwa ili tusipoteze pointi.”

Kwa upande wake, kocha wa Fountain Gate, Felix Minziro, amesema: “Timu yetu haina presha kwa sababu kila mtu anatarajia Simba ishinde. Hata hivyo, tumejipanga vizuri kuwashangaza watu katika uwanja wetu wa nyumbani, na lengo letu ni kupata pointi tatu muhimu.”


LIGI 01

AZAM VS MBEYA CITY

Azam itaingia katika mchezo huo ikiwa na lengo la kuendeleza ushindani wake katika ligi, huku Mbeya City ikihitaji matokeo mazuri ili kuimarisha nafasi yake katika msimamo.

Mchezo wa mwisho wa ligi kati ya timu hizo ulifanyika Aprili 9, 2026, katika Uwanja wa Sokoine na kumalizika kwa sare ya bila kufungana. Katika mchezo uliotangulia, uliofanyika Septemba 24, 2025, Azam FC ilipata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani.

Msimu huu, Azam imeonyesha uwezo wa kupata matokeo mazuri nyumbani na ugenini. Katika michezo yake ya ligi, iliifunga Namungo mabao 2-0, ikapoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Simba Septemba 16, na kuifunga Coastal Union mabao 2-0 Oktoba 9, 2026.

Akizungumzia mchezo huo, kocha wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema: “Nataka ushindi kwa sababu tunacheza katika uwanja wetu wa nyumbani. Tunalenga kumaliza katika nafasi za juu na kuwania ubingwa msimu huu, licha ya kuwaheshimu sana wapinzani wetu.”

Kwa upande wake, kocha wa Mbeya City, Salum Mayanga amesema timu yake imekuwa na matokeo ya kusuasua na baada ya michezo minane, imeshinda mitatu, sare moja na kupoteza minne, hivyo kujikusanyia pointi 10.

Hata hivyo, amesisitiza maandalizi ya kutosha yanaweza kuleta tofauti katika mchezo huo.

Katika mchezo mwingine wa leo, Coastal Union itakutana na Kagera Sugar katika Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga. Timu hizo zitaingia uwanjani zikisaka matokeo mazuri yatakayozisaidia kurejea katika mwenendo chanya baada ya kupata vipigo katika michezo yao ya hivi karibuni.