Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker afichua ugumu wa kuikabili Yanga

Muktasari:

  • Simba ni wenyeji wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga katika Ligi Kuu Bara, itakayopigwa kesho Jumapili Mei 3, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kuanzia saa 12 jioni.

KOCHA Mkuu wa Simba, Steve Barker, amesema ukitoa ubora wa wapinzani wao Yanga kwenye eneo la ulinzi, lakini wachezaji kama Pacome Zouzoua na Allan Okello ni hatari katika kushambulia.

Simba ni wenyeji wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga katika Ligi Kuu Bara, itakayopigwa kesho Jumapili Mei 3, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kuanzia saa 12 jioni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Barker amesema ili kushinda mechi hiyo, wanapaswa kufunga mabao jambo ambalo anaona sio rahisi kutokana na ubora wa wapinzani wao kwenye eneo la ulinzi.

"Ili kushinda mechi ya kesho tunapaswa kufunga magoli na sio rahisi, tumekuwa na muendelezo mzuri hiyo inafanya mechi hiyo kuwa ngumu kutokana na ubora wa Yanga kwenye eneo la ulinzi," amesema Barker na kuongeza.

"Kila mchezaji yuko sawa na wanashauku ya kutosha japo kushinda mechi dhidi ya Yanga ni ngumu na tunaelewa tukishinda kesho itakuwa tumepunguza gepu la pointi kubaki mbili dhidi ya Yanga, naamini itakuwa mechi ngumu kwa timu zote mbili."

Kwa upande wa beki wa kati wa Simba, Rushine De Reuck, amesema: "Tunataka kuwafanya WanaSimba wajivunie, sisi tunajua ugumu wa mechi ya kesho, hivyo tutapambana kupata matokeo mazuri."

Simba inaingia kwenye mechi hiyo ikiwa imetoka kuifunga Yanga bao 1-0 katika fainali ya Kombe la Muungano iliyochezwa Aprili 29, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.