Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker athibitisha Maema bado yupo Msimbazi

Muktasari:

  • Barker amesema pamoja na kuridhishwa na kiwango kinachoonyeshwa na wachezaji wapya walioungana na timu, bado kikosi chake hakijakamilika kwani kuna baadhi ya nyota wanaosubiriwa kuwasili kambini akiwemo Maema.

KIGALI: WAKATI mashabiki wa Simba wakiendelea kujiuliza kama kiungo mshambuliaji, Neo Maema, atakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao wa 2026/27 baada ya muda wake wa mkopo kufikia tamati, kocha wa kikosi hicho, Steve Barker, amethibitisha anatarajiwa kujiunga na kambi ya Wekundu wa Msimbazi siku chache zijazo.

Barker amesema pamoja na kuridhishwa na kiwango kinachoonyeshwa na wachezaji wapya walioungana na timu, bado kikosi chake hakijakamilika kwani kuna baadhi ya nyota wanaosubiriwa kuwasili kambini akiwemo Maema.

Kocha huyo amesema amevutiwa na kiwango cha mshambuliaji Ibrahim Doumbia, akieleza kuwa ameonyesha dalili za kuwa tishio kwa mabeki wa timu pinzani kutokana na nguvu alizonazo, kasi na uwezo wa kuwakabiliana na wapinzani.

Pia amempongeza beki Nathaniel Chilambo kwa kuonyesha utulivu akiwa na mpira, huku akimtaja Kelvin Nashon na Bakari Msimu ni wachezaji wanaoibeba kesho njema ya klabu hiyo.

"Tumefurahishwa na wachezaji tuliowaleta kuongeza nguvu kikosini, bado tunawakosa mmoja au wawili, kama Mpanzu na tunatumaini Neo Maema atajiunga nasi muda si mrefu. Kwa ujumla nimeridhishwa na maendeleo ya kikosi, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya na mambo mengi ya kuboresha kabla ya msimu kuanza," amesema Barker.

Kauli hiyo imeongeza matumaini kwa mashabiki wa Simba ambao wamekuwa wakisubiri kujua hatima ya Maema huku benchi la ufundi likiendelea kukiandaa kikosi chake kupitia michuano ya CECAFA Kagame kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa mashindano ya ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika.