Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pamba yamshusha bausi kutoka JKT Tanzania

Muktasari:

  • Beki huyo ambaye baba yake mzazi Seif Bausi ni kocha wa timu ya taifa ya Zanzi-bar ‘Zanzibar Heroes’ amelelewa katika mazingira ya soka kutokana na kipaji chake Simba iliwahi kuhitaji huduma yake msimu uliyopita lakini JKT Tz iliwawahi.

PAMBA Jiji imeendelea kuimarisha kikosi chake, kuhakikisha msimu ujao inarejea na ushindani wa juu, ikiwa tayari imemalizana na beki Abdulrahim Seif Bausi aliyeichezea JKT Tanzania msimu uliyopita.

Beki huyo ambaye baba yake mzazi Seif Bausi ni kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ amelelewa katika mazingira ya soka kutokana na kipaji chake Simba iliwahi kuhitaji huduma yake msimu uliyopita lakini JKT Tz iliwawahi.

Chanzo cha ndani kutoka Pamba kilisema, benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Francis Baraza, lilikuwa linamfuatilia Bausi likavutiwa na huduma yake ili iwe se-hemu ya kutumika katika timu hiyo kwa msimu ujao.

“Pamba lazima tukiimalishe kikosi, msimu unaoanza Agosti 14 utakuwa mgumu sa-na, timu zinasajili wachezaji wa maana na mechi zitakuwa zinachezwa karibu kari-bu, ukiachana na huyo Bausi kuna wachezaji wengi wapya wamejiunga na timu na wengine wameondoka,” kilisema chanzo hicho.

Bausi nje na soka ana Diploma ya Udhibiti na Uendeshaji wa Bandari, (Shipping and Port Management), aliisomea katika Chuo cha TPA, kilichopo Zanzibar alipoulizwa kuhusiana na usajili huo alijibu ni suala la Pamba kuzungumzia wachezaji wao.

Alipotafutwa kocha Baraza ili kuthibitisha hilo alisema:”Pamba tutatambulisha wachezaji, ila kwa sasa siwezi kumtaja mmoja mmoja, muda utakapofika mtawajua wote kama mlivyowaona baadhi yao katika mtandao wa timu.”

Miongoni mwa wachezaji ambao Pamba imewatangaza ni kiungo mkabaji raia wa Kenya, John Ochieng Champe kutoka Zanaco FC ya nchini Zambia.