Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika mpya atua Yanga

STRAIKA Pict


INADAIWA kwamba Klabu ya Yanga ipo hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Eswatini, Justice Figuareido kutoka Chippa United ya Afrika Kusini.


Awali, iliripotiwa Yanga ilikuwa ikimfuatilia Figuareido baada ya kocha raia wa Afrika Kusini, Manqoba Mngqithi, kutua kuinoa timu hiyo.


Na sasa taarifa mpya zinaeleza kuwa nyota huyo amewasili Dar es Salaam kutokea Afrika Kusini ili kukamilisha kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga.

“Makubaliano yamekamilika kwa kiasi kikubwa, kwa sababu klabu zote mbili tayari zimekubaliana, na Figuareido pia amekubali masharti binafsi ya mkataba,” kilisema chanzo kutoka Chippa United.

STRA 01

Figuareido ameichezea Chippa United kwa msimu mmoja pekee baada ya kujiunga nayo akitokea Richards Bay mwaka jana.

Katika kipindi chake akiwa Chippa United, amecheza mechi 28, huku akiwa Richards Bay akicheza jumla ya mechi 52.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, kocha Manqoba Mngqithi anamwona Figuareido kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika mpango wake wa kuijenga Yanga yenye uwezo wa kushindana na vigogo wa Afrika kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Licha ya fedha za kukamilisha dili hilo kutowekwa wazi, lakini vyanzo vinabainisha kwamba, uhamisho wa Figuareido kutoka Chippa United kwenda Yanga umegharimu Sh470 milioni.

Figuareido anayetumia zaidi mguu wa kulia ambaye kiasili ni mshambuliaji wa mwisho, pia ana uwezo wa kucheza winga zote mbili, kulia na kushoto.

Usajili wake ndani ya Yanga kama utafanikiwa, kuna jambo huenda likatokea ambalo ni mpango wa kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Laurindo Aurelio ‘Depu’ utakuwa unafanyika kwani hapo awali viongozi wa Yanga walikuwa na hesabu hizo.

STRA 02

Depu aliyetua Yanga Januari 2026, alimaliza msimu wa 2025-2026 akifunga mabao tisa katika Ligi Kuu ya NBC, huku ikielezwa hakufikia kiwango kilichotarajiwa wakati anasajiliwa.

Hatua hiyo ikawafanya mabosi wa Yanga kuingia sokoni kusaka mshambuliaji wa kuongeza nguvu katika eneo hilo kuelekea msimu ujao wa 2026-2027 huku ikichangiwa zaidi na kuondoka kwa Prince Dube, aliyefunga mabao kumi katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025-2026.

Katika kuimarisha eneo la ushambuliaji, Yanga tayari imemsajili mshambuliaji mwenye uraia wa nchi za Senegal na Ufaransa, Cheikh Ibrahima Toure.

Nyota huyo aliyejiunga na Yanga akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Al-Jabalain FC ya Saudi Arabia, msimu wa 2025-2026, alionyesha kiwango kizuri na kikosi hicho, kufuatia kufunga mabao 20 na asisti tano.

Pia Yanga imesajili viungo washambuliaji wa kimataifa wawili, Albert Kangwanda kutoka Red Arrows FC ya kwao Zambia, ambaye kwa msimu wa 2025-2026, alikuwa ni mchezaji bora wa msimu wa Ligi ya Zambia (MVP).

STRA 03

Katika Ligi Kuu ya Zambia msimu wa 2025–2026, Kangwanda alionyesha kiwango kizuri akiwa na Red Arrows FC kwa kufunga mabao 13, huku mashindano yote akihusika na mabao 25, kufuatia kufunga 17 na kuasisti manane.

Mwingine ni Housseine Zakouani aliyezaliwa Marseille, Ufaransa mwenye uraia wa Comoros aliyejiunga na kikosi hicho baada ya kuondoka Al-Zulfi SFC ya Saudi Arabia.

Toure, Kangwanda na Zakouani ni miongoni mwa wachezaji watatu wa kigeni waliotambulishwa na Yanga dirisha hili la msimu wa 2026-2027, wakiungana na nyota watano wazawa wakiwemo viungo washambuliaji, Juma Issa Abushiri aliyetoka Fountain Gate na Erick Mwijage kutoka KMC.

Wengine ni beki wa kulia, Abdulnasir Assa ‘Gamal’, beki wa kati, Mohamed Mussa, mshambuliaji, Hussein Juma Mihambo wote wakitokea Mashujaa, huku kiungo mshambuliaji, Suleiman Mbarouk ‘Mpemba D’ akitokea JKU FC ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa Rais wa Yanga, Hersi Said, Yanga imebakisha wachezaji saba wa kimataifa kutoka kikosi cha msimu uliopita 2025-2026, hivyo wanasajili watano kukamilisha idadi ya wachezaji 12 wanaotakiwa kikanuni. Katika hao watano, tayari watatu wametambulishwa.

Utambulisho wa wachezaji hao watatu wa kimataifa, inafanya Yanga kuwa nao kumi ambao ni Toure, Kangwanda, Zakouani, Djigui Diarra, Kouassi Attohoula Yao, Chadrack Boka, Duke Abuya, Maxi Nzengeli, Allan Okello na Depu.

Kiungo Muivory Coast, Pacome Zouzoua ameondolewa kwenye mfumo kwa muda ili kuuguza majeraha aliyoyapata katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya NBC 2025-2026 dhidi ya JKT Tanzania na kutarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu.