Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baum aanza kuzoea maisha Arsenal

BAUM Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo aliyejiunga na Arsenal amesema yupo tayari kukabiliana na ushindani mkubwa wa Ligi Kuu ya Wanawake England (WSL), akiamini uamuzi wa kujiunga na moja ya klabu kubwa duniani ni hatua sahihi kwenye safari yake.

WIKI moja tu ndani ya mazingira mapya ya London Kaskazini, lakini tayari kiungo mwenye asili ya Tanzania, Lisa Baum ameanza kuonyesha kiu ya kujifunza na kupambana katika maisha yake mapya ya soka.

Kiungo huyo aliyejiunga na Arsenal amesema yupo tayari kukabiliana na ushindani mkubwa wa Ligi Kuu ya Wanawake England (WSL), akiamini uamuzi wa kujiunga na moja ya klabu kubwa duniani ni hatua sahihi kwenye safari yake.

Baum ambaye alijiunga na Arsenal akitokea RB Leipzing ya Ujerumani, amekiri tangu anasaini mkataba na klabu hiyo alifahamu maisha yana presha kutokana na ukubwa wa jina la Arsenal na ubora wa ligi hiyo. 

BAU 01

Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye miaka 19 amesema changamoto hiyo ndiyo iliyomvutia zaidi na ndiyo sababu iliyomfanya akubali kuingia kwenye ushindani huo mkubwa.

"Napenda changamoto na ligi hii ni ngumu sana. Arsenal ni timu kubwa, lakini hilo ndilo lililonivutia zaidi nataka kujifunza, kukua na kuwa sehemu ya timu hii kubwa," amesema Baum.

Mchezaji huyo amesema licha ya kuwa ameishi London kwa muda mfupi, tayari ameanza kuzoea mazingira mapya ndani na nje ya uwanja. Kwa mujibu wake, uzoefu wa kuhamia klabu mpya hapo awali umemsaidia kutokupata wakati mgumu akiwa Arsenal.

BAU 02

"Nimekuwa hapa wiki moja sasa, lakini tayari nimeanza kuzoea mazingira. Kila ninaposaini klabu mpya huwa najitahidi kuzoea haraka kwa sababu najua hilo ni muhimu ili niweze kuonyesha uwezo wangu vizuri," amesema.

"Nina mengi ya kujifunza hapa. Kuna wachezaji bora, benchi la ufundi bora na mazingira ambayo yanaweza kunifanya niendelee kukua kama mchezaji," amesema kiungo huyo.

"Moyo wangu unaniambia hapa ni sehemu sahihi. Najua haitakuwa rahisi, lakini nimekuja hapa kwa sababu nataka changamoto hii na naamini ninaweza kufanya vizuri."

BAU 03

Baum alianza kucheza soka katika klabu za vijana za MTV Ahrensbök na baadaye TSV Pansdorf kabla ya kujiunga na akademi ya Hamburger SV mwaka 2021.

Akiwa HSV alisaidia timu ya vijana kutwaa ubingwa wa Ujerumani, kisha akapandishwa kikosi cha wakubwa na kuchangia kupanda kutoka Regionalliga hadi 2. Bundesliga na baadaye kufuzu Bundesliga ya wanawake.

Mwaka 2025 alijiunga na RB Leipzig, ambako alipata nafasi ya kucheza Bundesliga kwa mara ya kwanza alipocheza mechi 25 za ligi na kufunga mabao sita.