Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Coastal Union yataka kufufua msimu baada ya vipigo viwili

Muktasari:

  • Kauli ya kocha huyo inajiri baada ya timu hiyo kuanza mechi mbili za Ligi Kuu Bara kwa kuchapwa zote, ikianza na bao 1-0, dhidi ya wa maafande wa Mashujaa, Agosti 15, 2026, kisha kupoteza kwa kufungwa mabao 4-1 na Yanga, Agosti 20, 2026.

LICHA ya mwanzo mbaya katika Ligi Kuu Bara akiwa na Coastal Union, kocha mkuu wa timu hiyo, Fikiri Elias amesema bado wana nafasi ya kubadilisha mwenendo uliopo kwa sasa, hasa kutokana na changamoto za eneo la kujilinda na ushambuliaji.

Kauli ya kocha huyo inajiri baada ya timu hiyo kuanza mechi mbili za Ligi Kuu Bara kwa kuchapwa zote, ikianza na bao 1-0, dhidi ya wa maafande wa Mashujaa, Agosti 15, 2026, kisha kupoteza kwa kufungwa mabao 4-1 na Yanga, Agosti 20, 2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, Fikiri alisema mwenendo wa timu hiyo sio mzuri hasa baada ya kupoteza mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu Bara, japo bado hawajatoka katika malengo yao waliyojiwekea ya kuendelea kuonyesha ushindani kwa msimu huu.

“Tumeanza vibaya tofauti na matarajio yetu, kwa sasa hatuwezi kuangalia nyuma tena kwa sababu tuna mechi 28, mbele yetu za kurekebisha hali iliyopo kwa sasa, kikubwa ni umakini katika eneo la kujilinda na la ushambuliaji,” alisema Fikiri.

Kocha huyo alisema kuruhusu mabao matano katika mechi mbili sio jambo nzuri kutokana na ushindani uliopo, ila moja ya jambo kubwa analoendelea kulifanyia kazi ni kutengeneza balansi nzuri ya kiuchezaji kwa kuzingatia nyota wapya waliopo.

Timu hiyo ina kibarua kingine kesho Jumatatu cha kucheza dhidi ya TRA United kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga, huku ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa uwanjani hapo mara ya mwisho na maafande wa Mashujaa FC, bao 1-0, Agosti 15, 2026.

Coastal Union inaingia katika mechi hiyo ya tatu msimu huu na ya pili nyumbani, ikitafuta ushindi wa kwanza, kama ilivyo pia kwa TRA United iliyoanza kwa sare ya kufungana bao 1-1, dhidi ya JKT Tanzania, kisha kuchapwa na Azam FC mabao 2-1, ugenini kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.