Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Coastal Union yazindukia Arusha ikiichapa Polisi Tanzania

COASTAL Pict

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo, mshambuliaji wa Coastal Union, Maabad Maulid ndiye aliyeibuka shujaa kwa kikosi hicho, baada ya kufunga mabao mawili dakika ya 2 na 24 kwa mkwaju wa penalti, huku bao pekee la kufutia machozi kwa Coastal Union likifungwa na Anuary Jabir dakika ya 48.

TIMU ya Coastal Union imepata ushindi wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu, baada ya kuichapa Polisi Tanzania mabao 2-1, katika mechi ya mzunguko wa tano iliyopigwa leo Septemba 6, 2026 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.


Katika mechi hiyo, mshambuliaji wa Coastal Union, Maabad Maulid ndiye aliyeibuka shujaa kwa kikosi hicho, baada ya kufunga mabao mawili dakika ya 2 na 24 kwa mkwaju wa penalti, huku bao pekee la kufutia machozi kwa Coastal Union likifungwa na Anuary Jabir dakika ya 48.

Ushindi huo umefufua matumaini kwa Coastal Union inayofundishwa na Kocha Mkuu, Fikiri Elias, baada ya mwanzo mbaya wa kikosi hicho ambacho kabla ya leo kilikuwa kimechapwa mechi tatu na kutoka sare moja.

Timu hiyo ilianza msimu kwa kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa FC, Agosti 15, 2026, ikachapwa mabao 4-1 na Yanga, Agosti 20, 2026, ikatoka sare ya 1-1 na TRA United, Agosti 24, 2026, kisha ikachapwa 1-0 na Simba, Agosti 27, 2026.

COAS 01

Kwa upande wa Polisi Tanzania iliyorejea Ligi Kuu Bara msimu huu, kichapo cha leo ni cha pili baada ya mechi iliyopita kuchapwa mabao 4-2 dhidi ya Singida Black Stars, Agosti 29, 2026, kwenye Uwanja wa Airtel, Singida.

Kikosi hicho cha kilianza msimu huu kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC, Agosti 15, 2026, kisha ikashinda mechi mbili mfululizo kwa kuzifunga JKT Tanzania mabao 2-0, Agosti 20, 2026 na Dodoma Jiji ugenini bao 1-0, Agosti 25, 2026.

Kabla ya leo, mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana katika Ligi Kuu Bara ilikuwa Desemba 26, 2022, kwenye Uwanja wa Ushirika, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo zilifungana mabao 3-3.

COAS 02

Katika mechi hiyo mabao ya Polisi Tanzania yalifungwa na Ally Rutibinga dakika ya 10 na Kelvin Sabato aliyefunga mawili dakika ya 41 na 80, huku ya Coastal Union yakifungwa na Vicent Aboubakar dakika ya 18, Chilo Mkama akijifunga mwenyewe dakika ya 48 na Gustapha Saimon dakika ya 89.

Aidha, kabla ya leo, mara ya mwisho kwa Coastal Union kuifunga Polisi Tanzania katika Ligi Kuu Bara ilikuwa ni ushindi wa bao 1-0, Mei 8, 2022, lililofungwa na aliyekuwa nyota wa timu hiyo, Abdul Suleiman 'Sopu' dakika ya 21, anayeichezea kwa sasa Azam FC.

Kwa upande wa kikosi cha Polisi Tanzania, mara ya mwisho kuifunga Coastal Union katika Ligi Kuu Bara ilikuwa ni ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Deusdedit Cosmas dakika ya 51, Mei 16, 2021.

Matokeo ya leo yanaifanya Polisi Tanzania kushika nafasi ya saba na pointi saba, huku Coastal Union ikiwa nafasi ya 12 na pointi nne baada ya timu zote kucheza mechi tano.