Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Doumbia awashukuru mashabiki Simba

DOUMBIA Pict

Muktasari:

  • Katika mchezo huo ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, Doumbia aliingia katika kipindi cha pili lakini mashabiki wa timu hiyo waliweka bango kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo lililokuwa na ujumbe wa kumtia moyo mshambuliaji huyo raia wa Mali.

Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Doumbia amewashukuru mashabiki wa Simba kwa sapoti na mapenzi waliyomuonyesha katika mchezo wa timu hiyo dhidi ya Geita Gold, jana Jumatatu, Agosti 31, 2026.

Katika mchezo huo ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, Doumbia aliingia katika kipindi cha pili lakini mashabiki wa timu hiyo waliweka bango kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo lililokuwa na ujumbe wa kumtia moyo mshambuliaji huyo raia wa Mali.

“Leo (jana), niliposhuka kwenye basi, nilipata wakati ambao sitausahau kamwe. Nilipoona picha yangu kwenye bango lililoandikwa ‘TUKO PAMOJA DOUMBIA TUNAKUPENDA’.  Niliguswa sana moyoni. Kwa kweli, machozi yalinitoka.

“Katika soka, kuna nyakati ngumu, ushindi, kupoteza, lawama na nyakati za mashaka. Lakini leo (jana), mmenikumbusha jambo moja muhimu sana ambalo ni SIKO PEKE YANGU.

“Kwa mashabiki wote wa Simba, tafadhali mjue kwamba, bila kujali kitakachotokea, tayari mpo moyoni mwangu. Ninahisi upendo wenu, sapoti yenu na imani yenu kwangu. Na nawaahidi jambo moja, nitaendelea kufanya kazi, kupambana na kutoa kila nilichonacho kwa ajili ya jezi hii,” amesema Doumbia.

DOU 01

Doumbia amesema anajua kwamba anapita katika nyakati ngumu lakini atazishinda.

“Nyakati hizi ngumu, In Shaa Allah, tutazishinda pamoja. Kwa sababu familia haitelekezi mmoja wao wakati wa nyakati ngumu. Familia hubaki pamoja, huinuka tena na kusonga mbele kwa pamoja.

“Nataka kuwashukuru mashabiki wote wa Simba kote Tanzania. Wale wanaonitia moyo, wale wanaoniombea, wale wanaoniamini, lakini pia wale wanaonikosoa. Tafadhali jueni kwamba nawapenda nyote.

“Nyote mpo moyoni mwangu, kwa sababu maneno yenu, yawe mazuri au magumu kuyasikia, yananipa nguvu zaidi ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa bora zaidi,” amesema Doumbia.

Mshambuliaji huyo amesema ataendelea kufanya bidii ili awape furaha mashabiki wa timu hiyo na wote wanaomuunga mkono.

“Sitaki kuzungumza sana. Nataka kufanya kazi. Nataka kujifunza. Nataka kuboresha uwezo wangu. Nataka kupambana. Na muhimu zaidi, nataka kulipa upendo wenu uwanjani.

“Nyakati bora bado zinakuja, In Shaa Allah. Asanteni kwa kila kitu, familia yangu ya Simba. Asanteni kwa upendo wenu. Asanteni kwa uvumilivu wenu. Asanteni kwa sapoti yenu,” amesema Doumbia.

Mshambuliaji huyo raia wa Mali ameonekana kuwa katika wakati mgumu kutokana na kutoifungia Simba bao lolote katika mechi sita za mashindano ya ndani hapa nchini msimu huu.