Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fabrice Ngoy aigomea Namungo FC

Muktasari:

  • Mshambuliaji Ngoy msimu huu amefunga mabao nane mkataba wake unafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia Namungo kwa misimu mitatu.

UONGOZI wa Namungo FC 'Wauaji wa Kusini', umefikia makubaliano ya kutoendelea na mshambuliaji raia wa DR Congo, Fabrice Ngoy baada ya mkataba wake kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

Mshambuliaji Ngoy msimu huu amefunga mabao nane mkataba wake unafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia Namungo kwa misimu mitatu.

Ndoto za uongozi wa Namungo kumbakiza nyota huyo zimegonga mwamba baada ya mwenyewe kuamua kuachana nao ili akatafute changamoto mpya.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mratibu wa Namungo, Ally Suleiman alisema licha ya kutamani kuendelea na mchezaji huyo, ila ameamua kutokuwa tayari kusaini mkataba mpya, baada ya kueleza ni muda sahihi wa kuangalia changamoto sehemu nyingine.

"Sisi kama uongozi tumefanya jitihada za kumshawishi ili tuendelee naye msimu ujao lakini baada ya majadiliano ya muda mrefu ametutaarifu anataka kutafuta changamoto mpya, tulichokifanya ni kukubaliana na matakwa yake pia," alisema Ally.

Aidha, Ally alisema licha ya baadhi ya wachezaji wengine kumaliza mikataba yao pia mwisho wa msimu huu, ila mazungumzo yanaendelea kwa walio tayari kuongeza, japo malengo kwa sasa ni kuhakikisha wanamaliza vizuri mechi zilizobaki.

Nyota huyo ameaminiwa na kocha, Juma Mgunda licha ya uwepo wa washambuliaji wengine wakiongozwa na mkongomani mwenzake, Heritier Makambo aliyetoka TRA United zamani Tabora United na Abdulaziz Shahame 'Haaland', aliyetokea kikosi cha TMA FC.

Ngoy alijiunga na Namungo msimu wa 2023-2024, akitoka Kitayosce iliyobadilishwa jina na kuitwa Tabora United na sasa TRA United, baada ya kuifungia mabao 15 ikiwa Ligi ya Championship, nyuma ya kinara, Edward Songo wa JKT Tanzania aliyefunga 18.

Mshambuliaji huyo alitua hapa nchini kwa mara ya kwanza msimu wa 2022-2023, akitokea Real Nakonde FC ya Zambia na msimu wa 2023-2024, alifunga bao moja tu la Ligi Kuu, huku 2024-2025, akifunga mawili na msimu wa 2025-2026, amefunga manane