Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kachwele aondoka Vancouver Whitecaps

KACHWELE Pict

Muktasari:

  • Kachwele alicheza MLS NEXT Pro akiwa na Vancouver Whitecaps FC 2, kabla ya kupata nafasi ya kucheza MLS na baadaye kuhamia HFX Wanderers Ligi daraja la kwanza Canada kwa mkopo.

MSHAMBULIAJI wa Tanzania, Cyprian Kachwele amepewa mkono wa kwaheri na Vancouver Whitecaps FC 2 inayoshiriki Ligi daraja la tatu Marekani lakini inaelezwa kuna timu zimeanza kumfuatilia kuhitaji huduma yake.

Kachwele alicheza MLS NEXT Pro akiwa na Vancouver Whitecaps FC 2, kabla ya kupata nafasi ya kucheza MLS na baadaye kuhamia HFX Wanderers Ligi daraja la kwanza Canada kwa mkopo.

Whitecaps FC 2 ilitangaza Agosti 28, 2026 kuwa imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Kachwele kwa makubaliano ya pande zote. Kachwele, mwenye miaka 21 alijiunga na mfumo wa Vancouver mwaka 2023 akitokea Azam FC.

KACHWE 01

Taarifa ya upande wa Kachwele imeeleza kuwa kwa sasa bado si wakati sahihi kutaja klabu mpya kutokana na taratibu na makubaliano yanayohusiana na uhamisho huo, huku ikiwataka mashabiki na wadau wa soka kuwa na subira hadi taarifa rasmi itakapotolewa.

Lakini kwa taarifa ilizozipata Mwanaspoti ni kwamba kuna klabu mb ili za Ligi daraja la kwanza Canada zimeanza kuulizia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji huyo ambaye amekuwa na kiwango bora msimu uliopita.

“Bado hakuna mazungumzo ya kina lakini klabu zimevutiwa naye na tunaangalia uwezekano wa yeye kucheza,” amesema mmoja wa watu wa karibu wa mchezaji huyo.

Kachwele alitimkia Canada akitokea Azam FC mwaka 2023, ambako alikuwa amepitia akademi ya klabu hiyo na baadaye kupandishwa kikosi cha kwanza na timu ya vijana. Baada ya kujiunga na Vancouver Whitecaps FC 2, alianza kujenga jina katika MLS NEXT Pro, akicheza mechi 39 na kufunga mabao 11 na asisti mbili.

KACHWE 02

Msimu wa 2024, Kachwele alicheza mechi 20 za MLS NEXT Pro, akifunga mabao manne na kutoa asisti moja. Mwaka uliofuata alikuwa na kiwango bora, akicheza mechi 19, akifunga mabao saba na kutoa asisti nne.

Kachwele pia alipata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza cha Vancouver Whitecaps katika MLS. Klabu hiyo ilimpa nafasi ya kuanza kwenye baadhi ya mechi akianza mechi moja kwenye michezo mitatu aliyokuwa benchi.

Mwaka huu, Kachwele alipelekwa kwa mkopo HFX Wanderers akicheza mechi 15 za ligi, akifunga mabao mawili.