Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Keletso Makgalwa asema jambo zito Simba

KIALETSO Pict


WAKATI mashabiki wa Simba wakianza kuonesha kuvutiwa na kiwango cha Keletso Makgalwa licha ya kucheza kwa dakika 22 katika mchezo wa CECAFA Kagame Cup dhidi ya Mogadishu City uliomalizika kwa sare tasa (0-0), tayari kuna dalili kuwa kiungo huyo mshambuliaji wa Afrika Kusini anaweza kuwa kiungo muhimu katika kuifanya safu ya ushambuliaji ya Wekundu wa Msimbazi iwe na ladha tofauti msimu ujao.


Makgalwa ambaye ametua Simba akitokea Sekhukhune United ya Afrika Kusini akitambulishwa Jumamosi ya Julai 25, 2026, hakupewa muda mwingi katika mchezo huo wa kwanza, lakini kila alipogusa mpira alionyesha vitu vinavyoweza kuwafanya mashabiki wamkubali haraka kasi, uthubutu wa kumkabili beki mmoja baada ya mwingine na uwezo wa kufanya maamuzi kwa haraka.


Nyota huyo amesema yuko tayari kuipigania nembo ya Simba na kusaidia timu hiyo kushinda mataji.

“Nimekuja Simba kufanya kazi, kupambana kwa ajili ya timu na kushinda mataji. Nitajitolea kwa kila kitu kuhakikisha mashabiki wanafurahia kile nitakachokitoa uwanjani. Subirini muone,” amesema Makgalwa.

KALE 02

Kauli hiyo inaweza kuwa ya kawaida kwa mchezaji mpya, lakini tofauti itakuja kwenye utekelezaji.

Na dalili za mwanzo katika mchezo dhidi ya Mogadishu City zinaonesha kuwa Makgalwa anaweza kuwa mchezaji wa aina hiyo mwenye kujiamini, asiyeogopa kujaribu kitu tofauti na mwenye uwezo wa kufanya maajabu pale unapokuwa umekwama.

Ni aina ya mchezaji ambaye hafanyi mashambulizi yaonekane marefu. Anaweza kupokea mpira akiwa pembeni, akamvuta beki, akapunguza mwendo au akaongeza kasi ghafla na ndani ya sekunde chache akawa amefungua nafasi ya pasi au kupiga krosi.

Hiyo ndiyo sifa ambayo Simba imekuwa ikiihitaji kwa muda mrefu katika baadhi ya mechi, hasa inapokutana na timu zinazojilinda kwa wachezaji wengi nyuma ya mpira.

KALE 01

Makgalwa hakutua Simba akiwa mchezaji wa kawaida. Katika misimu miwili akiwa Sekhukhune United, alicheza mechi 66 za mashindano yote, akifunga mabao sita na kutoa asisti 20.

Takwimu hizo zinaonesha wazi kuwa nguvu yake kubwa si kufunga pekee, bali ni kuwafanya wenzake wafunge na hata katika mechezo wa juzi, alitengeneza nafasi moja.

Katika msimu wa 2024-2025 wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Makgalwa aliongoza kwa asisti akiwa na 11, rekodi iliyomweka miongoni mwa wachezaji wabunifu zaidi wa ligi hiyo.

Hilo ni jambo kubwa kwa Simba kwa sababu timu inaweza kuwa na washambuliaji wazuri, lakini kama hakuna mchezaji wa kuwafikishia mipira katika maeneo sahihi, ubora wao unaweza usionekane.

KALE 03

Ndiyo maana ujio wa Makgalwa unaweza kuifanya Simba iwe na sura mpya kabisa katika ushambuliaji. Sasa kocha Steve Barker anaweza kuwa na wachezaji kadhaa wa kigeni wanaoweza kucheza pembeni, kubadilishana nafasi na kuleta kasi tofauti kulingana na aina ya mpinzani.

Mbali na Makgalwa, Simba ina Elie Mpanzu, Anicet Oura na Libasse Gueye ambao msimu uliopita walikuwa na nafasi kubwa ya kucheza kikosi cha kwanza. Nyota hao kila mmoja ana kitu tofauti. Mpanzu anaweza kutumia nguvu na kasi yake kupenya upande wa kushoto au kulia.

Oura ana uwezo wa kucheza kwa ubunifu na kuingia katikati kutafuta nafasi huku Gueye anaweza kuongeza mwendo na mashambulizi ya kushtukiza huku Makgalwa akiwa mchezaji wa kutengeneza nafasi na kuunganisha mchezo.

Kocha Barker anaweza kutumia mfumo wa 4-3-3 au 4-2-3-1 na kupata faida ya kuwa na wachezaji wa pembeni wanaoweza kubadilishana nafasi bila kuharibu mpangilio wa timu.

Makgalwa anaweza kuanzia kulia, Mpanzu, Oura au Libasse kushoto, lakini baada ya dakika chache wakaingia katikati au kubadilishana upande, jambo linaloweza kuwachanganya mabeki wa wapinzani.

Hapo mchezaji wa aina ya Makgalwa anaweza kuwa na thamani kwa sababu hahitaji nafasi kubwa ili kutengeneza kitu. Anaweza kupiga chenga moja, akafungua nafasi ya pasi ya mwisho au akalazimisha faulo karibu na eneo la hatari.

Kitu kingine kinachoweza kuifanya Simba iwe tishio zaidi ni ushindani wa ndani ya kikosi. Makgalwa akianza vizuri, wachezaji wengine wa pembeni hawatakuwa na uhakika wa kucheza kila mechi.