Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha TRA amsifu Kamissoko

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Nyota huyo alicheza dakika 45, mechi ya Ligi Kuu Bara, TRA ikichapwa mabao 2-1, dhidi ya Azam FC, Agosti 20, 2026 na kuonyesha kiwango kizuri, jambo lililomfanya Ndayiragije kusifu uwezo wake wa kusoma vizuri mchezo.

KOCHA Mkuu wa TRA United, Mrundi Etienne Ndayiragije, amesifu kiwango kizuri kilichoonyeshwa na wachezaji wapya wa timu hiyo, huku akisema mshambuliaji Ousmane Kamissoko raia wa Mali akimtolea ana uwezo mzuri wa kuusoma mchezo.

Nyota huyo alicheza dakika 45, mechi ya Ligi Kuu Bara, TRA ikichapwa mabao 2-1, dhidi ya Azam FC, Agosti 20, 2026 na kuonyesha kiwango kizuri, jambo lililomfanya Ndayiragije kusifu uwezo wake wa kusoma vizuri mchezo.

Katika mechi hiyo, Kamissoko alichukua nafasi ya kiungo, Greyson Gwalala na kuifungia timu hiyo bao moja la dakika ya 45, baada ya Azam kutangulia kufunga kwa bao la Idd Seleman ‘Nado’ dakika ya nane na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 34.

Mbali na kufunga bao hilo, ila nyota huyo alichangia pia kwa kipa wa Azam, Aishi Manula kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 76, baada ya kuchezewa madhambi akiwa nje ya eneo la 18, wakati akiwa katika harakati za kwenda kufunga bao la pili.

Akizungumzia kiwango cha nyota huyo, Ndayiragije alisema wachezaji wote wapya wameonyesha kiwango kizuri na mwenendo wa kuvutia, licha ya kutopata ushindi katika mechi mbili, baada ya sare ya bao 1-1, dhidi ya JKT Tanzania, Agosti 16, 2026.

“Tumesajili kutokana na matakwa yetu na kuzingatia ubora wa wachezaji na nafasi tulizohitaji kufanyia maboresho, kwangu wote wameonyesha kiwango kizuri, ila ukimzungumzia Kamissoko alionyesha kile tulichokusudia kwake,” alisema Ndayiragije.

Nyota huyo alijiunga rasmi na TRA United, Julai 1, 2026, baada ya kuachana na TP Mazembe ya DR Congo, huku akiwa na uzoefu wa kucheza timu mbalimbali za Guidars FC na Stade Malien za Mali.