Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabondia waweka kambi Kigoma

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Zugo alisema kambi hiyo ni kwa ajili ya pambano la bondia wao Tatiana Ezekiel atakayepigana na Ignes Kayanga litakalopigwa Oktoba 25.

KOCHA Mkuu wa ngumi, Selemani Zugo amesema wamepanga kuweka kambi ya mwezi mmoja mkoani Kigoma, itakayoanza wiki ijayo kwa ajili ya kuwaandaa mabondia wao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Zugo alisema kambi hiyo ni kwa ajili ya pambano la bondia wao Tatiana Ezekiel atakayepigana na Ignes Kayanga litakalopigwa Oktoba 25.

Hivyo mabondia wengine watano watakuwa wanaendelea na mazoezi kwenye kambi hiyo lengo ni kumzindikiza bondia mwenzao.

Mabondia watakaokuwa kwenye kambi hiyo ni Ally Zugo anayeshindana uzito wa kilo 52, Mr Chunya kilo 49, Tatiana Ezekiel kilo 54, Sophia Hamisi kilo 51 na Jeniffer Zugo atakayepigana uzito wa kilo 57.

Aliongeza, mabondia hao wataendelea na mazoezi kujiandaa na pambano ambalo litatokea muda wowote.

Kwa mujibu wa Zugo, benchi la ufundi litakuwa chini yake akiwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na Dotto Zugo kama Kocha Msaidizi, huku Hamadi Tanga Adoswa akiwa Meneja wa kambi hiyo.

“Tutakuwa na kambi ya mwezi mmoja Kigoma kwa ajili ya kuwaandaa mabondia wetu. Tunataka kuhakikisha wanapata maandalizi mazuri na muda wa kutosha wa kufanya mazoezi,” alisema Zugo.

Mbali na maandalizi ya mabondia hao, Zugo alisema watatumia kambi hiyo kufanya uhamasishaji wa mchezo wa ngumi mkoani Kigoma kwa kushirikiana na gym mbalimbali zilizopo mkoani humo.

Alisema ushirikiano huo utawapa nafasi ya kukutana na mabondia wengine, kubadilishana uzoefu na pia kuhamasisha vijana wengi zaidi kuingia kwenye mchezo wa ngumi, huku akisisitiza kuwa lengo ni kuona Kigoma ikizalisha vipaji vipya.

“Tutafanya pia uhamasishaji wa mchezo wa ngumi mkoani Kigoma. Tutaungana na gym mbalimbali zilizopo mkoani humo ili kuufikisha mchezo kwa watu wengi na kuwapa nafasi vijana wenye vipaji,” alisema Zugo.