Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maema amchomoa kiungo Simba


HESABU za kiungo Neo Maema kurejea Simba zimehitimisha safari ya Mbotswana Mothusi Cooper ambaye ameshindwa kulishawishi benchi la ufundi baada ya kufanyiwa majaribio ya wiki moja kambini Rwanda.


Cooper, mwenye umri wa miaka 29, alijiunga na Simba wakati wa mashindano ya CECAFA Kagame, yanayotumiwa na timu hiyo kama sehemu ya maandalizi ya msimu mpya. Kiungo huyo alipata nafasi ya kucheza katika michezo miwili dhidi ya Mogadishu City na Jamus ambayo yote ilimalizika suluhu.

Hata hivyo, baada ya kushindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa, Mbotswana huyo alianza kuonekana nje ya mipango ya benchi la ufundi.

Hakushiriki mazoezi ya mwisho, Alhamisi,  kwenye kikosi kilichocheza mechi ya mwisho juzi hatua ya makundi dhidi ya Singida Black Stars kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali.

Habari ambazo Mwanaspoti imezipata zinaeleza kuwa nafasi ya Cooper ilitegemea hatma ya Maema. Simba ilikuwa ikimwangalia kama mbadala endapo mazungumzo ya kumrejesha kiungo huyo wa Afrika Kusini yasingefanikiwa.

Hata hivyo, kocha wa Simba, Steve Barker, aliliambia Mwanaspoti kuwa Maema anatarajiwa kujiunga na timu hiyo ndani ya siku chache zijazo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, jambo lililoweka wazi kuwa nafasi ya Cooper imefungwa rasmi.

Ujio wa Maema pia unafanya ushindani wa nafasi ya kiungo kuongezeka ndani ya Simba ambayo tayari dirisha hili la usajili imemsajili Ibraheem Jabaar  huku ikiwa na Kelvin Nashoon na Yusuph Kagoma katikati ya uwanja.

Taarifa zinaeleza Simba imefikia makubaliano na Mamelodi Sundowns kuendelea kupata huduma ya Maema, baada ya kuicheza kwa mkopo msimu uliopita.

Maema pia amethibitishia Mwanaspoti kuwa yupo mbioni kurejea nchini na anaamini msimu ujao utakuwa bora zaidi.

“Nipo kwenye hatua za kurejea, nina imani msimu ujao utakuwa mzuri zaidi kuliko uliopita,” alisema Maema.

Kiungo huyo alisajiliwa Simba msimu uliopita kwa mapendekezo ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids kabla ya kuondoka na kutua Raja Club Athletic. Licha ya mabadiliko ya benchi la ufundi, Maema aliendelea kuwa mmoja wa wachezaji waliomvutia Barker, akitoa mchango mkubwa katika mafanikio ya Simba kutwaa Kombe la Muungano na Kombe la CRDB msimu uliopita.

Kwa sasa, dalili zinaonyesha mlango wa Cooper umefungwa ramsi Msimbazi huku Maema akitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachotambulishwa kwenye tamasha la Simba Day pamoja na wachezaji wengine wapya.