Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MO apigiwa shangwe mkutano Simba 

MO Pict

Muktasari:

  • Mhasibu wa Simba Suleiman Kahumbu wakati akisoma ripoti ya mapato ya msimu uliopita amesema MO Dewji alichangia kiasi ha sh 4 Bilioni kwenye majeti yao ya mwaka ujao wa fedha.

WAKATI wanachama wa Simba wakisomewa ripoti ya mapato na matumizi, wameonyesha kukoshwa na rais wao wa heshima Mohammed Dewji 'MO' na namna anavyoipa fedha klabu hiyo.

Mhasibu wa Simba Suleiman Kahumbu wakati akisoma ripoti ya mapato ya msimu uliopita amesema MO Dewji alichangia kiasi ha sh 4 Bilioni kwenye majeti yao ya mwaka ujao wa fedha.

Mara baada ya Kahumbu kusema hivyo wanachama wa Simba wakiishangilia kwa nguvu huku wakipigia makofi taarifa hiyo.

Aidha Kahumbu akaendelea akisema katika bajeti ya msimu huu 2025-26, MO amechangia kiasi cha Sh 6 Bilioni kwenye bajeti yao.

Kahumbu akaongeza, fedha hizo za MO tayari zimeshaingizwa katika akaunti ya Simba ambazo ndio zimefanya usajili wa wachezaji wao msimu huu.

Baada ya kutangazwa hivyo wanachama hao tena wakashangilia kwa nguvu huku wakisimama na kuanza kuimba jina la Bilionea hiyo wakisema MO MO MO MO.