Monalisa kusalia Fountain Gate Princess
Muktasari:
- Beki huyo ambaye alijiunga na Fountain msimu uliopita akitokea Yanga Princess ambako alihudumu kwa misimu miwili mfululizochini ya kocha Mzambia, Charles Haalubono Monalisa na hakuwa anapata nafasi ya kuanza mara kwa mara kutokana na ushindani wa namba.
FOUNTAIN Gate Princess iko kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba beki wa kulia, Lucy Pajero 'Monalisa' baada ya mkataba wake wa awali kutamatika mwishoni mwa msimu huu.
Beki huyo ambaye alijiunga na Fountain msimu uliopita akitokea Yanga Princess ambako alihudumu kwa misimu miwili mfululizochini ya kocha Mzambia, Charles Haalubono Monalisa na hakuwa anapata nafasi ya kuanza mara kwa mara kutokana na ushindani wa namba.
Baada ya kukutana na changamoto hiyo alipomaliza mkataba wake aliamua kutafuta changamoto sehemu nyingine ndipo akajiunga na Fountain ambayo msimu huu umekuwa bora kwake.
Beki huyo aliisaidia Fountain kumaliza nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake ikikusanya pointi 37, kwenye mechi 22 imeshinda 11 sare nne na kupoteza mechi saba.
"Kocha na viongozi wanaamini bado ana mchango mkubwa kwenye kikosi ndiyo maana wameanza mapema kuhakikisha anabaki kabla ya msimu mpya kuanza," kilisema chanzo hicho.
Msimu uliopita Monalisa alikuwa miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango kikubwa katika safu ya ulinzi ya Fountain Gate Princess. Uwezo wake wa kuzuia mashambulizi, kupanda kusaidia mashambulizi na nidhamu ya mchezo ulimfanya kuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa tegemeo kwenye kikosi hicho.