Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtego wa Yanga Ligi Kuu

MTEGO Pict

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, leo wanaingia uwanjani kutegua mtego wa kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kukabiliana na JKT Tanzania.

Hii ni mechi ya raundi ya tatu iitakayopigwa leo Jumatatu Agosti 24, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12 jioni. Kisha Coastal Union na TRA United zitakutana saa 2:30 usiku kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na mwanzo mzuri wa msimu baada ya kuanza kampeni ya kutetea taji la ligi kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo ugenini, kabla ya kuichapa Coastal Union mabao 4-1 nyumbani. Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo kuingia kwenye mchezo wa leo ikiwa inajiamini, lakini kocha wake, Manqoba Mngqithi, anasisitiza kuwa hawapaswi kutazama matokeo ya nyuma ya JKT Tanzania.

Ushindi wa mechi mbili za kwanza ikifunga jumla ya mabao saba na kuruhusu mawili, uliiweka Yanga kileleni mwa msimamo, kabla ya Simba kushinda juzi na kuishusha ikifikisha pointi tisa. Yanga ikipata ushindi wa aina yoyote, itarejea kileleni.

MTE 02

“Matokeo ya JKT yaliyopita hayaakisi chochote kuelekea mchezo wetu. Nafahamu JKT wana mwalimu mzuri, kipa wao Chalamanda (Ramadhan) ni mzuri, Msengi (Ally) pamoja na Pascal Musa wako vizuri. Nawajua viungo wao kina Bajana (Sospeter) ni wachezaji wazuri na wanaweza kucheza mechi kubwa,” amesema Mngqithi.

Kwa upande wa JKT Tanzania, mambo hayajaanza kama walivyotarajia baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya TRA United katika mchezo wao wa kwanza waliocheza nyumbani, kabla ya kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania ugenini. Hata hivyo, kocha Ahmad Ally amesema hawana nafasi ya kujificha na wanatambua ukubwa wa kazi iliyo mbele yao.

“Tumetoka Arusha, tuna siku ya pili. Hatukawa vizuri kwa matokeo yaliyopita. Kama mwalimu najua jukumu gumu ambalo tuko nalo mbele yetu. Ni mechi ngumu kucheza na bingwa mtetezi, haiwezi kuwa rahisi kwetu na vilevile kwao,” amesema Ahmad.

MTE 01

Nahodha wa JKT Tanzania, Edward Songo, alikiri ugumu wa mchezo huo huku akisema kikosi chake kinajua maeneo kilipokosea katika michezo iliyopita na kinapaswa kurekebisha upungufu huo dhidi ya mabingwa hao.

“Haiwezi kuwa rahisi, muda mwingi tunapokutana na Yanga haijawahi kuwa mechi rahisi. Tunajua wapi tumekosea mechi zilizopita,” amesema Songo.

Kwa Yanga, mchezo huo pia utakuwa kipimo kingine kwa kikosi hicho baada ya kuanza msimu kwa matokeo mazuri.

Kipa wa Yanga, Aboutwalib Mshery anaamini ukaribu wa ratiba ndio unaofanya michezo kuwa na ugumu zaidi, akisema hakuna timu inayoweza kuchukuliwa kirahisi kutokana na matokeo yake ya nyuma.

MTE 03

“Mechi zipo karibu sana, haujawahi kuwa rahisi. Nadhani ndio kitu kinachofanya mechi kuwa ngumu zaidi kwa sababu timu inapopoteza haiwezi kuwa mechi rahisi,” amesema Mshery.

Katika mchezo wa pili utakaopigwa Mkwakwani, Coastal Union itakuwa mwenyeji wa TRA United kuanzia saa 2:30 usiku, ikiwa ni nafasi kwa timu hizo kutafuta ushindi wa kwanza wa msimu. Coastal imetoka kufungwa mabao 4-1 na Yanga, hivyo itakuwa na jukumu la kurejea kwa nguvu mbele ya mashabiki wake Tanga.

TRA United imeaanza vibaya baada ya kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya JKT Tanzania, kisha ikapoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Azam. Hivyo, mchezo wa Mkwakwani unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa kwa timu zote mbili, kila moja ikiwa na sababu ya kutafuta pointi tatu.

Mbali na matokeo, michezo hiyo miwili itatoa picha zaidi kuhusu nguvu za vikosi hivyo baada ya raundi mbili za mwanzo. Yanga itataka kuendeleza mwanzo wake mzuri na kuweka presha kwa wapinzani wake, wakati JKT Tanzania, Coastal Union na TRA United zitatafuta kurekebisha mwanzo wao na kuanza kukusanya pointi tatu.

MTE 04

REKODI ZAO

Yanga inaingia kwenye mchezo wa leo dhidi ya JKT Tanzania ikiwa na rekodi nzuri katika mechi 15 walizokutana, ambapo mabingwa hao hawajapoteza mchezo hata mmoja. Katika michezo hiyo, Yanga imeshinda mara 11 huku sare zikiwa nne, jambo linaloonyesha ubabe wao dhidi ya JKT katika miaka ya hivi karibuni. Mchezo wa mwisho uliozikutanisha timu hizo Juni 30, 2026, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 ugenini, ikiwa ni mfululizo wa matokeo mazuri dhidi ya wapinzani hao.

Rekodi hiyo inafanya mchezo wa leo kuwa na maswali mawili, je Yanga itaendeleza ubabe au JKT Tanzania itafurukuta mbele ya wananchi hao?

Katika mechi zao za mwisho, Yanga imeendelea kupata matokeo mazuri, ikiwemo ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT katika Kombe la Shirikisho Mei 16, 2026.

JKT sasa inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na nafasi ya kubadilisha historia hiyo, lakini kazi haitakuwa rahisi dhidi ya Yanga ambayo haijawahi kufungwa na timu hiyo katika mechi 15.