Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtihani wa kwanza KVZ Kagame Cup

KVZ Pict

Muktasari:

  • Mtihani huo wa KVZ kwa Rayon Sports ni katika michuano ya Kagame iliyoanza Julai 24, 2026 nchini Rwanda ambapo timu hizo zimepangwa kundi C lenye wapinzani wengine Al Hilal kutoka Sudan na Tusker ya Kenya.

KATIKA hesabu za KVZ kujiweka imara kuelekea msimu ujao wa 2026-2027 ambapo timu hiyo itaiwakilisha Zanzibar kimataifa, inaanza mtihani wake mbele ya Rayon Sports ya Rwanda.

Mtihani huo wa KVZ kwa Rayon Sports ni katika michuano ya Kagame iliyoanza Julai 24, 2026 nchini Rwanda ambapo timu hizo zimepangwa kundi C lenye wapinzani wengine Al Hilal kutoka Sudan na Tusker ya Kenya.

Kocha Mkuu wa KVZ ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Zanzibar msimu wa 2025-2026, Hababuu Ali, amesema kikosi chake kipo tayari kuikabili Rayon Sports.

HABA 02

Hababuu amesema, malengo yao katika michuano hiyo ni kujenga uzoefu wa mashindano ya kimataifa, hivyo ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

“Tumejipanga kucheza na Rayon, tunaamini tutafanya vizuri katika mchezo huu wa ufunguzi,” amesema kocha huyo.

Amesema, mashindano hayo ni fursa muhimu kwa wachezaji kupata uzoefu wa kucheza mechi za kimataifa na timu zenye ushindani mkubwa jambo litakalosaidia kuimarisha kikosi hicho.

Alibainisha kwamba, kupata mechi za ushindani katika kipindi kama hiki ni jambo zuri kwani ni mara chache kuzipata, hivyo watahakikisha wanaitumia fursa hiyo kujipima dhidi ya timu zenye ubora.

HABA 01

Alibainisha kuwa, benchi la ufundi limejipanga kuhakikisha timu inatoa ushindani katika kila mchezo, huku lengo likiwa si tu kupata matokeo mazuri bali kujenga kikosi imara kitakachokuwa tayari kwa changamoto za Ligi ya Mabingwa.

Matumaini makubwa ya KVZ ni wachezaji wapya waliowasajili kufanya vizuri ambapo hadi sasa imewatambulisha nyota 14 ambao ni Hamid Bakari Omar ‘Gaucho’, Nature Mwakilembe, Said Mussa ‘Mbeki’, Agustino Chalamba ‘Kaseke’, Muhammed Mussa Haji ‘Banega’, Mohammed Shaaban ‘Kwacha’, Hamad Ubwa ‘Baro’, Akram Muhina Omar ‘Haaland’, Munir Abdu Shafi ‘Mlipili’, Haruna Rashid Ali ‘Zaha’, Mudrik Abdi Shehe ‘Gonda’, Samir Khamis Said ‘Carragher’, Yakoub Said Mohd ‘Kane Ally’ na Suleiman Juma Kidawa ‘Pogba’.

Walioondoka ni Juma Shaban, Mussa Majuto, Raphaël Lucas, Mussa Jeba, Abdulhalim Pochink, Michael Joseph na Nassor Salum ‘Tiago’.

Baada ya kumalizana na Rayon ya Rwanda, Julai 29, KVZ itaikabili Al Hilal ya Sudan, kisha itamaliza makundi Agosti 1 kupambana na Tusker ya Kenya.