Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shikangwa, Mukandayisenga wana vita ya ufungaji

SHIKANGWA Pict

Muktasari:

  • Hadi mzunguko wa kwanza unatamatika Simba Queens inaongoza ligi na pointi 31 kwa tofauti ya pointi 11 na mpinzani wake JKT Queens mwenye 20 ikiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi tisa huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 30 zikitofautiana pointi moja.

NI kama vita ya ufungaji bora hadi raundi ya kwanza inamalizika imeachwa kwa washambuliaji wa kigeni wa watani wa jadi Simba Queens na Yanga Princess.

Hadi mzunguko wa kwanza unatamatika Simba Queens inaongoza ligi na pointi 31 kwa tofauti ya pointi 11 na mpinzani wake JKT Queens mwenye 20 ikiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi tisa huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 30 zikitofautiana pointi moja.

Achana na vita ya msimamo kwa timu hizo za Kariakoo lakini kuna vita nyingine ya chini chini inaendelea kwa washambuliaji wao, Jentrix Shikangwa wa Simba na Jeaninne Mukandayisenga wa Yanga.

SHIKA 01

Hadi sasa Mukandayisenga anaongoza kwenye orodha ya wafungaji akiwa na mabao 15 wastani wa kufunga bao moja kwa kila mechi.

Shikangwa ambaye ni msimu wake wa tatu kuitumikia ligi ya Tanzania akitokea Vihiga Queens ya nchini kwao Kenya, ana jumla ya mabao 10 akiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa wafungaji.

Hadi sasa katika ligi kuu ya wanawake zimefungwa Hat-trick sita kutoka kwa wachezaji wanne na wapinzani hao wawili wamefunga mbili kila mmoja.

SHIKA 02

Mukandayisenga alifunga hat-trick dhidi ya Fountain Gate Princess akifunga mabao matano peke yake Yanga ilipoondoka na ushindi wa mabao 5-4, nyingine alifunga dhidi ya Mashujaa Queens chama lake lilipoondoka na ushindi wa mabao 4-1.

Kwa upande wa Shikangwa alifunga dhidi ya Geita Queens na Bilo Queens Simba ikishinda mabao 4-0, wachezaji wengine wenye hat-trick moja moja ni Veronica Mapunda wa Mashujaa na Winifrida Gerald wa JKT Queens.