Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Songea United yaandika rekodi mbovu

SONGEA Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo ilipata ushindi wake wa kwanza kwa kuifunga Transit Camp mabao 3-2, Oktoba 30, 2026, baada ya kucheza mechi saba mfululizo bila ya ushindi, ikiwa ni rekodi ndefu tofauti na iliyowekwa na Hausung FC ya Njombe msimu wa 2025-2026.

KLABU ya Songea United iliyopo mjini Songea mkoani Ruvuma, imeandika rekodi mbovu zaidi ya kucheza mechi saba mfululizo za Ligi ya Championship msimu huu, bila ya ushindi, huku ikiivuka ya Hausung FC iliyoiweka msimu uliopita wa 2025-2026.

Timu hiyo ilipata ushindi wake wa kwanza kwa kuifunga Transit Camp mabao 3-2, Oktoba 30, 2026, baada ya kucheza mechi saba mfululizo bila ya ushindi, ikiwa ni rekodi ndefu tofauti na iliyowekwa na Hausung FC ya Njombe msimu wa 2025-2026.

Timu iliyokuwa inashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi bila ya ushindi tangu msimu uliopita wa 2025-2026, ilikuwa ni Hausung FC ya Njombe iliyocheza mechi tatu mfululizo, japo kwa Songea United imekuwa ni mpya kwa msimu huu wa 2026-2027.

Hausung FC iliyocheza Championship msimu wa 2025-2026, kisha kushuka msimu huo, iliifunga Stand United 'Chama la Wana' ya Shinyanga kwa mabao 3-0, ikiwa ni ushindi wa kwanza, baada ya kikosi hicho cha Njombe kuchapwa mechi tatu mfululizo.

Rekodi hiyo ya Hausung FC imevunjwa rasmi na Songea United, ambapo kikosi hicho chenye maskani yake mjini Songea mkoani Ruvuma, katika mechi nane iliyocheza imeshinda moja, sare tatu na kupoteza nne, kikishika nafasi ya 14 na pointi sita.