Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sowah afichua jambo Simba, autaja ubingwa

SOWAH Pict


MSHAMBULIAJI Jonathan Sowah, alifunga bao la pili msimu huu katika Ligi Kuu Bara katika mechi dhidi ya JKT Tanzania iliyochezwa Novemba 8, 2025, lakini akatoa kauli ya kibabe kwamba timu yao imeanza kuonyesha tabia za kibingwa na kutoa onyo kwa wapinzani.


Simba ilifanya 'comeback' ya kibabe mbele ya JKT Tanzania iliyotangulia kupata bao na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na kuifanya ifikishe pointi tisa ikiwa timu pekee iliyoshinda mechi tatu mfululizo hadi sasa kwenye ligi hiyo.


Awali Simba ilizifunga Fountain Gate na Namungo kwa mabao 3-0 kila moja na kukaa kileleni kwa kufikisha pointi tisa kabla ya leo kushushwa na Yanga.

Akizungumza na Mwanaspoti, Sowah aliyetua Msimbazi msimu huu kutoka Singida, amesema hatua ya kushinda ugenini kisha kupanda kileleni, tena wakitoka nyuma baada ya kutanguliwa bao la wenyeji JKT, ni ishara kwamba wameonyesha tabia ya timu inayoutaka ubingwa.

Sowah, ndiye aliyefunga bao la ushindi katika mechi hiyo akitokea benchi, baada ya Edward Songo kuitanguliza JKT kisha beki wa zamani wa maafande hao aliyetua Simba msimu huu, Wilson Nangu kuchomoa kipindi cha pili.

SOWA 01

Straika huyo Mghana aliyewahi kutamba na Madeama ya Ghana, amesema kitu ambacho kinavutia kwenye kikosi chao ni spiriti ya wachezaji na makocha kuamini kwamba kupoteza au kuangusha alama sio kitu stahiki kwao.

“Siyo rahisi kushinda mbele ya timu ambayo ilikuwa na matumizi makubwa ya nguvu kuliko mipango ya uwanjani, tena tunatoka nyuma, tunasawazisha na kupata ushindi, tunakwenda kuongoza ligi, hizi ni tabia za kibingwa ambazo hapa Simba tumeanza kuzionyesha mapema,” amesema Sowah na kuongeza;

“Ninapokuwa nasema tuna timu nzuri hii ndio maana yake unaona kila mchezaji na hata makocha wana shauku ya kuona tunashinda hata tukitangulia kuruhusu bao watu wanaona hatustahili kuwa nyuma, kuangusha pointi au kupoteza."

Sowah aliyemaliza msimu uliopita akiwa na mabao 13 ya Ligi Kuu kupitia mechi 15 tu, amesema wala hana shida sana na kuanzia bechi kwani anapata nafasi ya kuwasoma vizuri wapinzani.

Mshambuliaji huyo aliongeza, anataka kuhakikisha anaibeba Simba ambapo kama sio kutoa asisti basi afunge bao ili Simba iishi kwenye ndoto zake za kuchukua ubingwa.

SOWA 02

“Mimi sina shida hata kama kocha akiniambia nianzie benchi kazi yangu ni kuisadia Simba, nimekuwa natokea benchi lakini inanisaidia nawasoma mabeki wa upinzani wanafanya makosa yapi ili nikayatumie.

“Kila mtu kwenye hii timu anaishi na malengo kwamba tunautaka ubingwa na mwendo huo unaanzia kama hivi, kazi yangu ni kuendelea kufunga kila nikipata nafasi bila kujali ni muda gani nitakuwa uwanjani kama sio kufunga basi nitengeneze mwenzangu ashinde.

Kwa sasa Simba inajianda na mechi ya kwanza ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro Atletico ya Angola itakayopigwa kati ya Novemba 21 na 23, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kabla ya kuifuata Stade Malien wiki moja jijini Bamako, Mali kwa mechi ya pili na hatua hiyo, mnyama ikipangwa Kundi D.