Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Twiga Stars kutupa karata ya kwanza

TWIGA Pict

Muktasari:

  • Licha ya Afrika Kusini kuingia ikiwa mabingwa wa Afrika na moja ya timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo, Tanzania inaingia ikiwa na matumaini makubwa ya kuandika historia mpya.

TWIGA Stars leo inaanza kutupa karata yake ya kwanza katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON 2026) kwa kuvaana na mabingwa wa Afrika, Banyana Banyana ya Afrika Kusini, katika mechi ya Kundi C, itakayopigwa saa 4:00 usiku kwenye Uwanja wa Moulay Rachid, Casablanca.

Licha ya Afrika Kusini kuingia ikiwa mabingwa wa Afrika na moja ya timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo, Tanzania inaingia ikiwa na matumaini makubwa ya kuandika historia mpya.

Historia inaonyesha timu hizo zimekutana mara mbili katika fainali za WAFCON, mwaka 2010 na 2024, huku Banyana Banyana ikishinda mechi moja na sare moja.

TWIG 01

Mwaka 2010, Afrika Kusini ilishinda mabao 2-1, huku bao pekee la Tanzania likifungwa na mshambuliaji Esther Chabruma, ambaye sasa ni sehemu ya benchi la ufundi la Twiga Stars. Miaka 14 baadaye kwenye WAFCON 2024, Tanzania ilionyesha ushindani mkubwa zaidi na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya wapinzani hao.

Rekodi hiyo inaipa Twiga Stars sababu ya kuamini inaweza kuondoka na angalau pointi mbele ya mabingwa hao, hasa ikizingatiwa kuwa sehemu ya benchi la ufundi la sasa linaifahamu vizuri Banyana Banyana kutokana na uzoefu wa muda mrefu wa mashindano haya.

TWIG 02

Mbali na mechi hiyo, nyingine ya kundi B itakayopigwa itawakutanisha timu za Afrika Magharibi kati ya Ivory Coast dhidi ya Burkina Faso.

Nahodha wa Stars, Opah Clement anayekipiga SD Eibar ya Ligi Kuu Hispania ataongoza safu ya ushambuliaji ya Tanzania kwenye mechi hiyo na kumbukumbu zinaonyesha mechi ya mwisho nyota huyo alifunga bao dhidi ya Banyana Banyana.

TWIG 03

Akizungumzia mechi hiyo Opah amesema "Tunajua tunakutana na mechi ngumu lakini kwa upande wetu tumejiandaa vizuri na tunaamini kile tulichofundishwa na kocha tutaenda kukifanyia kazi."