Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujumbe wa balua baada ya kurejea Uarabuni

BALUA Pict

Muktasari:

  • Balua ametoa ahadi hiyo baada ya klabu hiyo kukamilisha taratibu za kumsajili kwa ajili ya msimu mpya, akirejea katika kikosi hicho baada ya kuitumikia kwa mkopo msimu uliopita.

RIYADH, SAUDI ARABIA: KIUNGO wa Tanzania, Edwin Balua, ameahidi kufanya kazi kwa bidii pamoja na wachezaji wenzake ili kuonyesha kiwango bora baada ya kurejea katika klabu ya Al-Entisar ya Saudi Arabia.

Balua ametoa ahadi hiyo baada ya klabu hiyo kukamilisha taratibu za kumsajili kwa ajili ya msimu mpya, akirejea katika kikosi hicho baada ya kuitumikia kwa mkopo msimu uliopita.

Akizungumza baada ya kutambulishwa, Balua ameushukuru uongozi wa Al-Entisar pamoja na benchi la ufundi kwa kumuamini na kumpa nafasi nyingine ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

“Nitafanya kazi kwa bidii pamoja na wachezaji wenzangu ili kuonyesha kiwango bora cha kiufundi na kuifanya timu iwe katika hali nzuri mbele ya kila mtu,” amesema Balua.

Kiungo huyo amerejea Al-Entisar baada ya kuitumikia kwa mkopo wa miezi sita kuanzia Januari 2026 akiwa mali ya Simba.

Hata hivyo, wakati Simba ikijiandaa na msimu huu wa 2026-2027, ilitangaza Balua ni miongoni mwa wachezaji ambao hawataendelea nao akiwa tayari amemaliza mkataba wake.

Balua aliyetua Simba Januari 2024 akitokea Tanzania Prisons, kabla ya sasa kurejea Al-Entisar, aliichezea Enosis Paralimniou ya Cyprus pia kwa mkopo wa miezi sita kuanzia Agosti 2025.

Al-Entisar ni klabu inayotokea Rabigh, katika Mkoa wa Makkah, Saudi Arabia. Klabu hiyo ilianzishwa mwaka 1978, imekuwa ikishiriki katika Saudi Second Division, ambayo ni daraja la tatu katika mfumo wa ligi ya soka nchini humo.

Kwa msimu wa 2025-2026, Al-Entisar ilikuwa miongoni mwa timu 32 zilizoshiriki Second Division, katika droo ya msimu huo iliwekwa Kundi A pamoja na timu kama Al-Ain, Al-Jeel, Al-Sha'la, Al-Najran na Al-Rawdah.

Uzoefu huo wa awali unaifanya safari ya Balua sasa kuwa tofauti, kwani tayari anafahamu mazingira ya klabu, ligi na wachezaji wenzake ndani ya Al-Entisar.