Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga mdogo mdogo, yaikazia JS Kabylie kwao

YANGA Pict

Muktasari:

  • Suluhu hiyo imeifanya Yanga kufikisha pointi nne baada ya mechi mbili, kwani awali ikiwa nyumbani ilishinda bao 1-0 dhidi ya AS Far Rabat ya Morocco kwenye Uwanja wa New Amaan Zanzibar ambayo usiku wa leo walikuwa uwanjani kuumana na vinara wa kundi hilo Al Ahly.

YANGA imeendelea kuweka hai tumaini la kutinga robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya usiku wa leo Novemba 28, 2025 kuongeza pointi moja katika Kundi B ikiwabana JS Kabylie ya Algeria nyumbani kwao kwa kutoka suluhu katika mechi ya pili ya michuano hiyo.

Suluhu hiyo imeifanya Yanga kufikisha pointi nne baada ya mechi mbili, kwani awali ikiwa nyumbani ilishinda bao 1-0 dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar ambayo usiku wa leo ipo uwanjani kuumana na Al Ahly.

Tofauti na matarajio ya wengi kwamba Yanga huenda ingekuwa na wakati mgumu katika kundi hilo kutokana na kupangwa na vigogo watupu kutoka Afrika ya Kaskazini, wawakilishi hao wa Tanzania wamethibitisha kwa sasa wamekomaa kwa kuendelea kukusanya pointi, lakini ikiupiga mpira mwingi.

YANG 01

Katika mechi hiyo iliyocheza kwenye Uwanja wa Hocine Ait Ahmed, Yanga iliwabana wenyeji ambao walipoteza mechi ya kwanza kwa mabao 4-1 mbele ya Al Ahly, ila umakini mbovu uliinyima kutoka na ushindi wa pili.

Yanga Ikicheza kwa utulivu ikitengeneza nafasi ya kwanza nzuri dakika ya sita tu kupitia shambulizi la adhabu ndogo, shuti la winga Celestin Ecua likapanguliwa na kipa Mohammed Hadid.

Wenyeji walitengeneza nafasi nzuri ya kwanza dakika ya 14 kupitia shambulizi la kona, kichwa cha beki Zineddine Belaid kikagonga mwamba wa juu na kurudi uwanjani.

Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu, Yanga ikifika tena lango la JS Kabylie dakika ya 16 Ecua akipenyezewa pasi ndefu na Pacome Zouzoua inamkuta eneo zuri lakini shuti lake hafifu linadakwa kirahisi na Hadid.

YANG 02

Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu Yanga ikifika tena lango la JS Kabylie dakika ya 16 Ecua akipenyezewa pasi ndefu na Pacome Zouzoua inamkuta eneo zuri lakini shuti lake hafifu linadakwa kirahisi na Hadid.

Kabylie nayo ikatengeneza nafasi nyingine dakika ya 18 kupitia mshambuliaji wake Aymen Mahious kinatoka nje kidogo akipokea krosi ya beki wake wa kulia.

Hadi mapumziko timu hizo zilitoka bila kufungana huku Yanga ilionyesha kucheza kwa ubora mkubwa.

Kipindi cha pili timu zote zilirudi na mabadiliko wenyeji wakimtoa kiungo Babacar Sarr nafasi yake ikichukuliwa na mlinzi Mostapha Bott.

YANG 03

JS Kabylie nayo ikatengeneza nafasi nyingine dakika ya 18 kupitia mshambuliaji wake Aymen Mahious kinatoka nje kidogo akipokea krosi ya beki wake wa kulia.

Hadi mapumziko timu hizo zilitoka bila kufungana huku Yanga ikionyesha kucheza kwa ubora mkubwa.

Kipindi cha pili timu zote zilirudi na mabadiliko wenyeji wakimtoa kiungo Babacar Sarr nafasi yake ikichukuliwa na mlinzi Mostapha Bott.

Yanga nayo ikamtoa kiungo wake Mudathir Yahya nafasi yake ikichukuliwa na Mohamed Doumbia ikilenga kuongeza kasi ya pasi za kwenda mbele. Hadi mwisho matokeo 0-0.


YANG 04


PEDRO ANAJUA

Kwa namna Yanga inavyocheza imethibitisha kocha Pedro Goncalves ambaye aliichukua timu hivi karibuni akimpokea Romain Folz.

Matokeo hayo yameifanya Yanga kuendelea kuboresha rekodi zake katika michuano ya CAF kwani ilikuwa haijawahi kuanza na ushindi katika makundi, ikiwamo msimu uliopita ilipopteza mechi mbili za kwanza mbele ya Al Hilal na MC Alger, lakini kwa sasa imekusanya pointi nne.

Akianza na kikosi kilekile kilichocheza mechi iliyopita, Pedro aliingia na mbinu za kushambulia kwa akili na nidhamu na kuwafanya wenyeji kushindwa kufanya maajabu.

Kwa matokeo hayo Yanga imekusanya pointi nne sasa na inasubiri hadi mwakani kucheza mechi mbili mfululizo dhidi ya Al Ahly ambao baadae kidogo ipo ugenini Morocco kuumana na maafande wa AS FAR Rabat.