Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bruno: Ronaldo bado ni alama ya Ureno

BRUN 02

Muktasari:

  • Ronaldo (41), aliondoka kambini baada ya Kocha Jorge Jesus kumwambia hatakuwa katika kikosi cha kwanza dhidi ya Denmark kwenye Ligi ya Mataifa, mchezo ambao Ureno ilishinda mabao 4-2 bila uwepo wa nahodha huyo.

LISBON, URENO: KIUNGO wa Manchester United na timu ya taifa ya Ureno, Bruno Fernandes amesema Cristiano Ronaldo bado ni alama kubwa zaidi ya soka nchini hiyo licha ya kuondoka kambini baada ya kufahamishwa kwamba hatakuwa kwenye kikosi cha kwanza.

Ronaldo (41), aliondoka kambini baada ya Kocha Jorge Jesus kumwambia hatakuwa katika kikosi cha kwanza dhidi ya Denmark kwenye Ligi ya Mataifa, mchezo ambao Ureno ilishinda mabao 4-2 bila uwepo wa nahodha huyo.

Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid na Manchester United ndiye kinara wa mabao na mechi kwa Ureno, akiwa amefunga mabao 146 katika mechi 234. Pia aliisaidia nchi yake kutwaa Euro 2016 na Ligi ya Mataifa mara mbili.

BRUN 03

Hata hivyo, kuondoka kwake kambini kumeibua maswali kuhusu hatma yake katika kikosi hicho.

Fernandes amesema: “Nilizungumza na Cristiano na nilichomwambia, ambacho pia narudia hapa, ni kwamba bila kujali kitakachotokea, Cristiano Ronaldo hataacha kuwa alama kubwa zaidi ya timu yetu ya taifa, soka letu na nchi yetu kutokana na yote aliyoyafanya, si Ureno pekee bali duniani kote.

“Anastahili nafasi miongoni mwa wachezaji bora wa muda wote na pia katika mioyo ya Wareno wote. Cha muhimu ni kuacha kugawanyika.

“Hakuna mgawanyiko ndani ya timu ya taifa. Sisi ni kitu kimoja na tutaendelea kuwa hivyo licha ya kelele zinazoweza kutoka nje.

BRUN 03

“Cristiano ndiye na ataendelea kuwa ikoni kubwa zaidi ya timu yetu ya taifa. Anastahili heshima ya kila mtu, bila kujali nani anampenda zaidi au kidogo.”

Ureno ilitwaa Ligi ya Mataifa mwaka 2019 na ni mabingwa watetezi baada ya kuifunga Hispania kwa penalti katika fainali ya mwaka 2025, kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 120, huku Ronaldo akifunga bao moja.

Katika michuano hiyo, Ureno ilianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wales, huku Ronaldo akicheza dakika 67, kabla ya kuwa benchi bila kutumika katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Norway.

Baada ya mechi hizo, Ronaldo aliondoka kambini kabla ya mchezo dhidi ya Denmark.

Kocha Jesus, ambaye aliwahi kumfundisha Ronaldo katika klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia, alichukua nafasi ya Roberto Martinez kwenye timu hiyo.

BRUNO Pict

Baada ya mechi tatu, Ureno inaongoza Kundi A ikiwa na pointi tisa, kabla ya mechi yake ya jana dhidi ya Norway jijini Porto.

Jesus amesema Ronaldo ni “alama ya Ureno”, lakini akasema atazungumzia zaidi suala hilo baada ya mchezo dhidi ya Norway.

“Nitaangalia zaidi timu na mpinzani wetu ambaye ni Norway, moja ya timu tano bora barani Ulaya. Hilo ndilo tatizo tulilonalo kwa sasa,” amesema Jesus, mwenye umri wa miaka 72.