Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Habari njema Man United, Baleba aanza kuonekana baada ya jeraha

Muktasari:

  • Baleba, aliyesajiliwa na United kutoka Brighton kwa ada ya Pauni 70 milioni dirisha la majira ya kiangazi, bado hajacheza mechi rasmi kwa kikosi hicho baada ya kuanza msimu akiwa na jeraha la kifundo cha mguu.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imepata habari njema baada ya kiungo wake mpya, Carlos Baleba, kuonekana uwanjani katika mechi ya kirafiki iliofanyika katika uwanja wa mazoezi wa Carrington.

Baleba, aliyesajiliwa na United kutoka Brighton kwa ada ya Pauni 70 milioni dirisha la majira ya kiangazi, bado hajacheza mechi rasmi kwa kikosi hicho baada ya kuanza msimu akiwa na jeraha la kifundo cha mguu.

Hata hivyo, matumaini ya mashabiki kumuona akivaa jezi ya United yameongezeka baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kushiriki katika mchezo dhidi ya Lausanne-Sport ya Uswisi.

Baleba alikuwa kwenye benchi wakati United ilipolazimishwa sare ya 1-1 na Fulham kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa, lakini hakupata nafasi ya kuingia uwanjani.

Kocha wa United, Michael Carrick, aliwahi kusema Baleba alikuwa akifanya kila juhudi kurejea uwanjani haraka iwezekanavyo.

Kurejea kwa Baleba kunatajwa kuwa habari muhimu kwa United, hasa wakati klabu hiyo ikikabiliwa na wasiwasi wa majeruhi kwa baadhi ya wachezaji wake kipindi hiki cha mapumziko ya wiki tatu ya mechi za kimataifa.

Kiungo na nahodha Bruno Fernandes alikosa mrchi ya Ureno dhidi ya Norway kutokana na jeraha, ingawa baadaye alipona na kuanza katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Norway.

Kocha wa Ureno, Jorge Jesus, alieleza tatizo la Fernandes ni jeraha "gumu" katika eneo la mguu wa chini.

Kwa upande mwingine, beki Noussair Mazraoui aliondoka uwanjani akiwa anachechemea wakati Morocco ilipocheza dhidi ya Lesotho katika mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mazraoui aliumia baada ya kuingia kwenye harakati za kuwania mpira dakika ya 68, akatua vibaya na mara moja kuashiria kwa benchi kwamba alikuwa akihisi maumivu makali.

United pia imekosa huduma za Marcus Rashford na Kobbie Mainoo, ambao walijiondoa kwenye kikosi cha England kabla ya mapumziko ya kimataifa.


ji wengine wanaoendelea kufuatiliwa kutokana na hali zao za kiafya ni Amad Diallo, Benjamin Sesko na Patrick Dorgu.


MTIHANI DHIDI TOTTENHAM

United inatarajiwa kurejea kwenye mashindano baada ya mapumziko hayo Oktoba 10, itakapokuwa mwenyeji wa Tottenham Hotspur katika dimba la Old Trafford.

Kurejea kwa Baleba kwenye mazoezi ya ushindani kunaweza kumpa Carrick chaguo jingine muhimu katika kikosi chake, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona lini kiungo huyo mpya atafanya debut yake rasmi.