Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yamgeukia Endrick Madrid

Muktasari:

  • Enrick ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika kikosi cha Lyon amekuwa akisisitiza kwamba anataka kuendelea kubakia Real Madrid ili kupigania namba katika kikosi cha kwanza, ambacho kwa sasa kimesheheni mastaa wa maana zaidi

LIVERPOOL imeulizia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Endrick, mwenye umri wa miaka 20, kutoka Real Madrid baada ya Brighton kukataliwa kwa ofa ya pili waliyoituma kwa winga wa kimataifa wa Gambia, Yankuba Minteh, mwenye miaka 22.

Enrick ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika kikosi cha Lyon amekuwa akisisitiza kwamba anataka kuendelea kubakia Real Madrid ili kupigania namba katika kikosi cha kwanza, ambacho kwa sasa kimesheheni mastaa wa maana zaidi.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba huenda watu wa karibu wa mchezaji huyo wakamshauri aondoke ili kwenda Liverpool au timu nyingine ambako atapata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza kuliko kubaki Madrid inakoelezwa kwamba nafasi yake ya kucheza inaweza kuwa ndogo zaidi msimu ujao hasa baada ya kuwasili kwa Yan Diomande kutoka RB Leipzig.

Endrick alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Brazil kilichoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 ambako hata hivyo hakuonyesha maajabu makubwa kutokana na kutokuwa na namba ya kuanza kikosini, akianzia benchi na mara chache alizopata fursa hakuna alichofanya.

Mchezaji huyo pia ana ofa nyingi mezani kutoka katika timu za Ligi Kuu Italia na Ufaransa.


Nicolas Jackson

CHELSEA inatarajia Aston Villa itawasilisha ofa kwa ajili ya mshambuliaji wake wa kimataifa wa Senegal, Nicolas Jackson, mwenye miaka 25, ambaye imepanga kumuuza kwa Pauni milioni 65. Hata hivyo, mkwanja unaohitajika huenda usikubaliwe na Villa inayomthaminisha kwa bei ya nusu ya hiyo.


Victor Osimhen

ARSENAL bado ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Galatasaray, Victor Osimhen, mwenye miaka 27, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria atalazimika kupunguza madai yake ya mshahara ili dili hilo litimie. Inaelezwa kwamba dai la mshahara mkubwa zaidi ya ule anaoupokea Uturuki linaweza kuwa kikwazo iwapo atakomaa.


Christopher Nkunku

NEWCASTLE United na RB Leipzig zinaendelea na mazungumzo na AC Milan kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa, Christopher Nkunku, mwenye miaka 28. Timu hizo mbili zinaweza kufanikiwa ikiwa tu Milan itaamua kuachana na mpango wa kumnga'ang'ania mchezaji huyo.


Julian Alvarez

ATLETICO Madrid imekubali kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Julian Alvarez, kwenda Arsenal, lakini mchezaji huyo mwenye miaka 26 amekataa uhamisho huo akisisitiza kuwa anataka kujiunga na Barcelona pekee. Uamuzi wake unaweza kuwa kikwazo cha kuondoka kwake kwani Atletico haitaki kumuuza LaLiga.


Jules Ahoka

SUNDELAND inadaiwa kufikia makubaliano ya Pauni 4 milioni ili kumsajili kiungo wa timu ya taifa ya DR Congo chini ya miaka 23, Jules Ahoka, mwenye miaka 20, kutoka Royal Antwerp. Nyota huyo ambaye hajawahi kucheza timu yoyote nchini kwao anaweza kutua Englanda wakati wowote.


Michele Di Gregorio

BOURNEMOUTH iko katika hatua za mwisho za kumsajili kipa wa Juventus, Michele Di Gregorio, mwenye miaka 29, kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua moja kwa moja baadaye.


Willy Kambwala

BEKI wa kati wa DR Congo, Willy Kambwala, mwenye miaka 21, yuko mbioni kujiunga na Como akitokea Villarreal. Klabu yake ya zamani, Manchester United, inatarajiwa kunufaika kupitia kipengele cha asilimia ya mauzo ya baadaye kilichowekwa kwenye mkataba wake.


Daniel Munoz

NYOTA wa Colombia anayecheza kama beki wa pembeni anayekipiga Crystal Palace, Daniel Munoz, mwenye miaka 30, anahusishwa na uhamisho kwenda Tottenham Hotspur, lakini ripoti zinaeleza kuwa mchezaji huyo ameanza kuwa na shaka kuhusu kujiunga na Spurs.


Wilfried Gnonto

WINGA wa Leeds na timu ya taifa ya Italia, Wilfried Gnonto anaweza kuuzwa katika dirisha hili la usajili ili timu hiyo ipate fedha kwa ajili ya kusajili nyota ambao amekuwa ikipambana kuhakikisha wanatua kikosini.