Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man city yauza timu nzima kwa Pauni 475 milioni

MAUZO Pict

Muktasari:

  • Guardiola aliondoka Etihad baada ya miaka 10 akiwa kwenye benchi, huku nafasi yake ikichukuliwa na aliyekuwa msaidizi wake, Enzo Maresca, aliyerejea katika klabu hiyo aliyosaidia kutwaa Treble miaka mitatu iliyopita.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City imeachana na kikosi cha nyota kinachoweza kuunda timu nzima yenye thamani ya takribani Pauni475.2 milioni, katika kipindi ambacho klabu hiyo inapitia mabadiliko makubwa baada ya kuondoka kwa kocha Pep Guardiola.

Guardiola aliondoka Etihad baada ya miaka 10 akiwa kwenye benchi, huku nafasi yake ikichukuliwa na aliyekuwa msaidizi wake, Enzo Maresca, aliyerejea katika klabu hiyo aliyosaidia kutwaa Treble miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo, kikosi ambacho sasa kinapewa jukumu la kuirejesha City kwenye kilele cha Ligi Kuu England kinaonekana tofauti kabisa na kile alichokiacha Guardiola.

Ikiwa uhamisho unaotarajiwa utakamilika kabla ya dirisha kufungwa Jumanne usiku, City inaweza kuwa imepoteza wachezaji wa kutosha kuunda kikosi kamili cha wachezaji 11, ambao kwa pamoja waligharimu klabu hiyo Pauni milioni 475.2 waliposajiliwa.

MAUZ 01

TRAFFORD AONDOKA, STONES AACHWA

Golikipa wa kikosi hicho ni James Trafford ambaye City ilimrudisha kutoka Burnley mwaka mmoja uliopita kwa Pauni27 milioni, lakini ameshaondoka tena, akijiunga na Leeds kwa Pauni40 milioni.

Safu ya ulinzi ina John Stones, ambaye City ilimsajili kwa Pauni47.5 milioni na kuwa mmoja wa wachezaji wake waliodumu kwa muda mrefu.

Stones ameondoka baada ya mkataba wake kumalizika, hali iliyomfanya aendelee kuchezea England wakati akiwa hana klabu.

Manuel Akanji na Nathan Ake pia wameondoka. Akanji alisajiliwa kwa Pauni milioni 15.1, huku Ake akigharimu Pauni41milioni.

Akanji amejiunga moja kwa moja na Inter Milan baada ya awali kwenda kwa mkopo, wakati Ake amehamia Fenerbahçe kwa Pauni8.5milioni.

Safu hiyo ya ulinzi inakamilishwa na Kalvin Phillips, ambaye City ilimsajili kwa Pauni45 milioni.

Ingawa Phillips hajaondoka moja kwa moja kwa sababu amejiunga na Sheffield United kwa mkopo, ni mkopo wake wa nne tangu mwaka 2024 na bado ana miaka miwili kwenye mkataba wake wa City.

Hali hiyo inaashiria wazi kuwa hayupo kwenye mipango ya klabu hiyo na kuna uwezekano mkubwa asicheze tena kwa City.

MAUZ 02

RODRI NA VIUNGO WENGINE

Safu ya kiungo ina majina mazito, ikiongozwa na Rodri ambaye anaelekea Barcelona.

City imemuuza kiungo huyo kwa Pauni65.4 milioni, ikiwa ni zaidi kwa Pauni 2.9 milioni ya fedha ilizotumia kumsajili kutoka Atletico Madrid mwaka 2019.

Nico Gonzalez pia anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake kwenda Newcastle kwa Pauni52 milioni, ikiwa ni faida ya Pauni milioni mbili kwa City baada ya kumsajili Februari 2025.

Tijjani Reijnders naye amedumu msimu mmoja pekee City. Alisajiliwa kutoka AC Milan kwa Pauni46.5 milioni  na sasa anatarajiwa kuondoka kwenda Al-Qadsiah kwa Pauni milioni 52.

MAUZ 03

SAVINHO NA MARMOUSH WAKIMBILIA LONDON

Katika safu ya ushambuliaji, Savinho ni miongoni mwa walioondoka baada ya kuhamia Tottenham kwa dili la Pauni85 milioni.

City ilimsajili Mbrazil huyo kutoka klabu dada ya Troyes kwa Pauni33.6 milioni mwaka 2024, huku akionekana kama mrithi wa Riyad Mahrez.

Omar Marmoush pia anatarajiwa kujiunga na Tottenham, licha ya kusajiliwa na City kutoka Eintracht Frankfurt kwa Pauni64 milioni Januari mwaka jana.

Bernardo Silva anakamilisha kikosi hicho cha wachezaji wanaoondoka.

Mchezaji huyo wa Ureno alitumia miaka tisa City baada ya kusajiliwa kutoka Monaco kwa Pauni43 milioni mwaka 2017, kabla ya kuondoka kama mchezaji huru na kusaini mkataba wa miaka miwili na Real Madrid.


PAUNI 234 MILIONI KUNUNUA

Licha ya kuondoka kwa nyota hao, City imejaribu kusawazisha kikosi kwa kutumia takribani Pauni 234 milioni kusajili wachezaji wapya.

Sehemu kubwa ya fedha hizo imetumika kumsajili Elliot Anderson kwa Pauni116 milioni na kijana Ayyoub Bouaddi kwa Pauni81.4 milioni.

Hata hivyo, matumizi hayo yanaweza kuongezeka kwa zaidi ya Pauni100 milioni iwapo City itafanikiwa kumnasa kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez.

Hivyo, kipindi hiki kinaonekana kuwa mwanzo wa sura mpya kwa Manchester City, huku Maresca akipewa jukumu la kujenga upya kikosi baada ya kuondoka kwa Guardiola na kundi kubwa la wachezaji waliokuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya klabu hiyo katika miaka ya nyuma.