Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hamisa atuma ujumbe mzito, amtaja Aziz KI

MOBETO Pict

Muktasari:

  • Amesema amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz, uhusiano huu ulikuwa na hekaheka za watu wa kwenye mitandao ya kijamii na nje ya mitandao kuwafuatilia kila uchao.

MWANAMITINDO na mjasiriamali maarufu wa Tanzania, Hamisa Mobetto, amesema hajawahi kutikiswa na mwanamke yeyote kiasi cha kukosa usingizi kwa kuhofia kuibiwa mwanaume.

Akizungumza na Mwanaspoti Hamisa amesema siku zote mwanamke anatakiwa kujiamini kuwa hakuna neno la kusikia litakalomtikisa au kumnyima usingizi.

“We naye ushaanza na maswali yako, ila nikwambie tu maneno maneno kuhusu kwenye  uhusiano wangu kabla sijaingia kwenye ndoa hayajawahi kuninyima usingizi kwa sababu ninajiamini, yaani kiufupi mimi ni mwanamke jasiri,” amesema Hamisa.

Amesema amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz, uhusiano huu ulikuwa na hekaheka za watu wa kwenye mitandao ya kijamii na nje ya mitandao kuwafuatilia kila uchao.

Uhusiano huu pia ulidaiwa kupata upinzani kutoka kwa wanafamilia wa Diamond Platnumz hadi ikadaiwa alitimuliwa nyumbani na kuacha wigi alipokuwa ameenda kulala kwa supastaa huyo wa muziki wa kizazi kipya ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume, Naseeb Jr.

Mbali na uhusiano huo, Hamisa pia amezaa na Mkurugenzi wa EFM Majizo, huu pia ulikuwa uhusiano wenye hekaheka baada ya DJ huyo wa zamani kuachana na Hamisa na kwenda kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na Elizabeth Michael 'Lulu'.

Hata hivyo, kwa sasa Hamisa ameolewa na nyota wa zamani ya klabu ya Yanga, Stephane Aziz KI, anayecheza Wydad Casablanca ya Morocco. Ndoa yao ilifungwa Februari 16, 16,2025.