Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Insp. Haroun agoma kuacha muziki, atoa sababu

INSPEKTA Pict

Muktasari:

  • Inspector Haroun, ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa Bongo waliopata kufanya vizuri upande wa Hip Hip akitamba na makundi kadhaa ikiwamo Gangwe Mobb lililoanza mwaka 1993/94 akiwa na mwenzake, Luteni Kalama baada ya kuvutiwa zaidi na LWP Majitu.

ZIMEPITA siku chache tangu mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Haroun Rashid Kahena a.k.a Inspekta Haroun au Babu kufunga mwaka 2025 kwa kuachia ngoma mbili mpya ‘AI’ (Akili Mnemba) na ‘Maisha Ndio Haya Haya’, huku akiweka bayana sababu ya ‘kugoma’ kuacha muziki.

Inspector Haroun, ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa Bongo waliopata kufanya vizuri upande wa Hip Hip akitamba na makundi kadhaa ikiwamo Gangwe Mobb lililoanza mwaka 1993/94 akiwa na mwenzake, Luteni Kalama baada ya kuvutiwa zaidi na LWP Majitu.

Inspector Haroun katika mahojiano na Mwanasapoti, amezungumzia masuala ya muziki na nje ya muziki na pia kutohofia kuachia nyimbo kwa wakati huu ambao watu wajiitao Gen-Z, kufanya kampeni ya watu wasisapoti kazi za wasanii.

INSP 01

MSIKIE MWENYEWE

“Mimi sina tatizo na wananchi wenye itikadi zote, naishi nao vizuri sana, na sisi Temeke tunavyoishi tunaishi na watu wa aina zote hivyo sijakutana na hilo vuguvugu.

“Watu wengi wamekuwa na fikra za kuwa, wanamuziki wa zamani  hawataki kuwa na menejiment kitu ambacho sio kweli, vitu haviwezi kwenda bila menejimenti, mimi nina mtu na watu ambao wananisimamia ila siwezi kuwataja hapa lakini wana mchango mkubwa sana kwangu, na hapa ninavyokwambia nina mpango wa kufungua live band, tayari nimeshanunuliwa vyombo kwa ajili ya kufanya kazi.

“Sababu mimi ni mwanamuziki ambaye naweza kuimba live bendi na hata kutumia vyombo tu, hapo utachagua mwenyewe utakayenihitaji unataka nikutolee burudani ya  gani.”

“Mpango wa pili ni kuwa na studio kwa ajili ya kurekodi, yaani  kuwa na rekodi lebo kwa ajili ya wanamuziki wenye vipaji kuja kurekodi, Watanzania kuna watu wengi wana vipaji, na mipango ya tatu  ni kuwaletea muendelezo wa burudani, kama hivi ikitoka EP inakuja albamu, ambayo imesheheni wanamuziki wengi wa TMK na wa sehemu nyingine.”

INSP 02

NYIMBO 100 SIKU TANO

“Mimi nina kipaji cha kuandika nyimbo mia moja kwa siku tano, na hapa sijafikiria kustaafu kwani naona bado sijautendea haki muziki na bado mashabiki wananihitaji.”

Kuhusu kufanya kazi na wasanii wa kike, Babu anasema; “Ukiniambia niseme wanamuziki wa kike wenye kufanya vizuri katika uimbaji, wote wanafanya vizuri tunaona ushindani wa tasnia ya muziki wetu.”

INSP 03

KAZI ZAKE MPYA

Inspector Haroun ambaye aliwahi kutingisha muziki wa kizazi kipya kwa ngoma kali kama Mtoto wa Geti Kali na Asali wa Moyo, amesema, lengo la kutoa nyimbo mbili kwa pamoja ni kwa ajili ya kuwapa zawadi mashabiki zake ambao kwa wale wa Hip Hop watafurahia wimbo wa ‘AI’ (Akili Mnemba) na wale mashabiki wa Amapiano watafurahishwa na wimbo wa ‘Maisha Ndio Haya Haya’.

“Lengo la kuachia nyimbo hizi mbili ni kwa ajili ya kuwapa zawadi mashabiki zangu, na ndio maana zipo kwenye mahadhi tofauti, moja AI ni mahadhi ya Hip-Hop, Maisha Ndio Haya Haya ina mahadhi ya Amapiano

“Hivyo nina imani mashabiki zangu watafurahishwa na hii zawadi, sababu kwa mwaka huu mwezi wa Julai nilitoa wimbo wa ‘Final Sub’ niliomshirikisha Ibraah, ambao mahadhi yake ni Hip-hop, sasa ukiangalia hadi sasa imepita miezi mitano bila kutoa nyimbo, ndio maana nasema hii ni zawadi kwa mashabiki wangu,” amesema Inspector Haroun.