Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bravo mwanetu Foba! Kinachohitajika sasa ni mwendelezo tu

Muktasari:

  • Ripoti ambazo kijiwe imezipata ni kwamba Yakoub atakosa mechi zote zilizosalia za mashindano hayo kwa hivyo sasa Taifa Stars imebaki na makipa wawili ambao Zuberi Foba na Hussein Masalanga.

TANZANIA ilipata ghafla pigo siku chache kabla ya mechi yake ya kwanza ya Fainali za AFCON 2025 dhidi ya Nigeria baada ya kipa namba moja wa Taifa Stars katika mashindano hayo, Yakoub Suleiman kuumia.

Ripoti ambazo kijiwe imezipata ni kwamba Yakoub atakosa mechi zote zilizosalia za mashindano hayo kwa hivyo sasa Taifa Stars imebaki na makipa wawili ambao Zuberi Foba na Hussein Masalanga.

Swali likabakia nani atadaka katika mechi dhidi ya Nigeria kati ya bwa’mdogo Foba na Masalanga maana wote wawili hawana uzoefu wa kusimama langoni katika mechi za kimashindano za timu ya taifa.

Hatimaye benchi la ufundi likaamua kuanza na Foba katika mechi hiyo ambao tulipoteza kwa mabao 2-1, shukrani kwa bao letu pekee lililofungwa na Charles M’mombwa.

Hata hivyo, pamoja na kupoteza mechi hiyo ya kwanza, Foba alicheza vizuri sana kwa kufanya vitu vingi vya msingi ambavyo kipa anatakiwa avitekeleze ndani ya uwanja.

Aliokoa hatari kama nane hivi za Nigeria ambazo nusu au robo yake tu zingejaa nyavuni maana yake Taifa Stars tungekuwa hivi sasa ndio timu iliyoruhusu idadi kubwa ya mabao katika raundi ya kwanza.

Alianzisha vyema mipira na alikuwa akiipanga na kuikumbusha timu majukumu mara kwa mara kana kwamba ni kipa ambaye tayari ameshacheza idadi kubwa ya mechi za Stars kumbe ndio mechi yake ya kwanza.

Jambo la muhimu kwa Foba hivi sasa ni kuhakikisha kile alichokifanya dhidi ya Nigeria kinaendelea ili azidi kuwa kipa tegemeo kwa nchi na klabu yake ya Azam.

Kwa umri na uzoefu wake mdogo, ategemee kama atafanya makosa, lakini yasiwe sababu ya yeye kurudi nyuma bali yamuimarishe zaidi.