Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kama masikhara Mnyama ameipeleka dabi Mbweni

JICHO Pict


MNYAMA ameamua kuupeleka mpira Mbweni. Pambano la Simba na Yanga litachezwa Mbweni kwa mujibu wa mwenyeji wa pambano Simba. Kwanza kabisa hatupaswi kuhoji, ni haki yao ya msingi. Uwanja wa Meja David Isamuhyo utaandaa moja ya mechi ambazo zitaamua ubingwa msimu huu. Utaanda Dabi ya Kariakoo, Simba dhidi ya Yanga.


Kwanza kabisa itakuwa mechi ya kwanza ya dabi kuchezwa Kinondoni. Haijawahi kutokea. Wakati Dabi kadhaa zikiwa zimechezwa mikoani, hakuna dabi ambayo imewahi kuchezwa Kinondoni. Dabi zimechezwa Arusha, Mwanza,  Mbeya, Dodoma, Morogoro na Zanzibar lakini hakuna dabi imechezewa Wilaya ya Kinondoni.


Dabi zilikuwa zinachezwa Ilala na Temeke katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Na sasa Mnyama ametupeleka Mbweni katika pambano lake muhimu la ligi kuu.

Kwa nini ametupeleka Mbweni? Nimetabasamu kidogo. Kwanza kabisa ni nongwa. Matumizi halali ya haki yao ambayo yanaambatana na nongwa juu yake. Kwamba wanaweza kuamua kucheza popote pale kwa sababu wao ni wenyeji na wana haki ya kuamua wapi kwa kucheza.

Yanga walikuwa na haki katika pambano la kwanza ambalo walikuwa wenyeji wakaamua kwenda zao Zanzibar.

Kwa nini Simba wasitumie haki yao ya uenyeji kwenda kucheza Mbweni? Wamefanya kitu sahihi kwao ingawa mashabiki wamelalamika uwanja ni mdogo kuchezwa pambano la Simba na Yanga. Yanga hawapaswi kufungua mdomo wao kwa namna yoyote ile ingawa maamuzi ya Simba yanaacha maswali mengi nyuma yake.

JICH 01

Simba wangeweza kucheza Mwanza au Arusha baada ya uwanja wa Mkapa kufungiwa lakini wameamua tu kupunguza mashabiki kwa kucheza Mbweni.

Sio tu wamepunguza mashabiki wa Yanga, pia wamewapunguza mashabiki wao wenyewe. Mashabiki wa Simba. Uwanja ni mdogo kwa pande zote mbili. Hata kama Simba wakiamua wajae wenyewe tu bado hawawezi kumbabaisha mpinzani. Idadi ya mashabiki itakuwa ndogo.

Ninachohisi ni Simba wameamua kutengeneza ngome yao pale kwa Meja Jenerali Isamuhyo. Kwamba Yanga wanahisi ngome yao kuu katika pambano la dabi ni Unguja.

Simba wameanza kutuaminisha ngome yao kuu katika dabi inaweza kuwa Mbweni. Tatizo hawawezi kutuaminisha vema kama hawajamfunga mtani katika uwanja huo.

Bado uwanja wa Mbweni unabakia kuwa wa kila mtu. Wote ni wageni. Hata hivyo Simba wana nafasi kubwa ya kutuaminisha uwanja wa Mbweni ni ngome yao kama watamfunga mtani.

JICH 02

Awali walikuwa wanajaribu kutuaminisha uwanja wa Mkapa ni ngome yao dhidi ya Yanga katika miaka ya karibuni lakini historia haisemi hivyo. Mara nyingi walizofungwa mfululizo katika miaka ya karibuni wamefungwa kwa Mkapa.

Tumekumbuka kitu? Ndiyo. Simba wamebana meno na kutumia haki yao ya msingi kama ambavyo hivi karibuni Azam walitumia. Azam walikwenda kucheza Chamazi pambano dhidi ya Simba na waliweka kiingilio cha Sh15,000.

Simba kupitia kwa mmoja kati ya mabosi wao, Crescentius  Magori walitaka Azam ichunguzwe kwa kuhujumu mechi. Kwamba kwa nini waliweka kiingilio kikubwa ili kuzuia maskini wasije uwanjani.

Natazamia pia Simba wataweka kiingilio kikubwa kwa ajili ya kuzuia watu wengi wasiende uwanjani. Uwanja mdogo mechi kubwa, timu kubwa. Lazima mechi iwe ghali.

Wakati ule Arsenal wakicheza Uwanja wa Highbury kiingilio kilikuwa kikubwa kwa sababu timu yao ni kubwa na uwanja ulikuwa mdogo. Mahitaji ya kuona mechi yalikuwa makubwa huku idadi iliyohitajika ikiwa ndogo.

Kwa Simba hii sio mechi ya kiuchumi kwao. Wangetaka pesa nyingi wangekwenda Mwanza au Arusha. Hapana. Kuna sinema fulani ya kukomoana inaendelea. Kama sio kukomoana basi ni kujaribu kujenga imani mpya 'kwa IsamuHyo hatoki mtu'. Ndani ya hii imani kuna mambo mawili ambayo yanaweza kutokea.

JICH 03

Kama Simba wakishinda basi uwanja wa Isamuyo utaabudiwa na mashabiki wao. Bahati mbaya tu hawataweza kucheza mechi za kimataifa hapo lakini watakuwa na imani kubwa Kwa Isamuhyo sasa ni uwanja wa nyumbani.

Jambo la pili ni kama wakifungwa mabosi wa timu watakuwa na kesi kubwa kwa mashabiki. Kwanza utakuwa umewanyima wengi burudani ya kwenda kuangalia mechi halafu bado umefungwa.

Njia pekee ya kuhalalisha maamuzi ya kwenda uwanja wa Isamuhyo ni kushinda mechi dhidi ya mtani. Vinginevyo itaonekana yalikuwa maamuzi ya ajabu.

Utakuwa umekosa vyote. Umekosa pesa, umekosa matokeo na umekosa imani kutoka kwa mashabiki. Maamuzi haya yanafanya pambano hilo liwe moja kati ya mechi za dabi za kuvutia. Fikiria Yanga watasema nini wakishinda Isamuhyo. Watatukana na kukejeli zaidi.

Awali Yanga walitukana sana wakati Clement Mzize alipofunga bao la pili katika pambano la dabi ambalo waamuzi walitoka nje kuja kuchezesha. Ilionekana kama vile dabi ilikuwa ya moto zaidi na haki ilihitajika zaidi na TFF wakaamua kuleta waamuzi kutoka Misri.

Bado Mnyama alikufa mabao mawili katika lango la kusini pale Kwa Mkapa. Safari hii watasema tulikwenda sebuleni kwao Isamuhyo na tukashinda mechi.

Nani mwingine atanufaika? Kuna mtu amekaa kando na atanufaika zaidi. Azam TV. Mashabiki wengi watajikatia tamaa kwenda uwanjani na watalazimika kukaa nyumbani kwao kutazama mechi hii.

Watalazimika kulipia ving'amuzi vyao vya Azam TV.  Hata wale wa mikoani wanaokodi mabasi kuja Dar es salaam kutazama dabi, naamini safari hii hawatafanya hivyo.

Dabi imeshushwa hadhi? Sina uhakika sana na hilo. Dabi ya Kariakoo itaendelea kuwa na hadhi yake.

Siungani sana na wanaosema hivyo. Hili ambalo Simba wamefanya litaendelea kuwa miongoni mwa matukio ya kihistoria ya dabi yenyewe. Itabakia kuwa historia tu kama ile hat trick ya King Abdala Kibadeni 'Mputa' dhidi ya nyavu za Yanga mwaka 1977.

Kama tunavyokumbuka hat trick ya Kibadeni dhidi ya kipa Suleiman Jongo wa Yanga ndivyo tutakavyokumbuka siku moja Simba waliwahi kutupeleka Mbweni kucheza dabi.

Wakati mwingine utata unaifanya dabi izungumzwe zaidi. Kama ule utata wa 'hatuchezi' unaifanya dabi izungumzwe zaidi. Kule kwenye sanaa kuna kitu kinaitwa kiki. Kwamba unatengeza mazingira ya kuzungumzwa kuliko kazi yenyewe. Kama ambavyo tupo hapa tunajadili maamuzi ya Simba kupeleka mechi Mbweni karibu na bahari.

Ambacho ninatamani ni pambano lenyewe lisiishe kwa sare. Mmoja afungwe ili tujue yalikuwa maamuzi ya kijinga kupeleka dabi Mbweni au yalikuwa maamuzi ya kishujaa kupeleka dabi eneo hilo. Sare itasababisha kila mtu aongee kitu ambacho hatukipendi. Mmoja afungwe ili mji usipoe.

Kitu cha kufikirika ni kama Yanga wanaweza kupewa nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja huo siku moja kabla ya mechi. Itachekesha kidogo kuona kama watazuiwa.

Hapana. Hata wakizuiwa wana timu ya kwenda kesho yake na kushinda mechi. Labda tu wakiamua kuleta nongwa. Wenzao wakati ule wakichomoa kucheza mechi kwa sababu hiyo walikuwa wametafuta upenyo tu wa kuchomokea. Walishaona mambo ni nagumu.