Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pep Guardiola kama Julius Caesar alikuja, aliona, alitawala

PAZIA Pict


JULIUS Caesar, mtawala wa Warumi miaka hiyo. Baada ya kushinda vita yake kwa urahisi tu dhidi ya utawala wa Zela alitamka maneno haya katika barua aliyomuandikia seneta wa Warumi. Niliona, nilikuja na nilitawala.


Unawezaje kumzuia Pep Guardiola asiseme maneno hayo wakati huu anaondoka ligi kuu ya England? Ni kweli. Anaweza kusema tu kwamba ‘Aliona, alikuja na alitawala. Ni kama ilivyokuwa kwa Julius Caesar.


Anaondoka zake Manchester City kifua kikiwa mbele na macho yakitazama mbele zaidi. Misimu hii miwili Pep hajaondoka na taji la ligi kuu ya England lakini aliitazama ligi kuu ya England, akaja, akaingia na kuiweka katika mikono yake.

Pep alikuwa Hispania kule. Alianzisha mpira wake. Alitawala. Baadae alienda zake Ujerumani. Akawapeleka mpira wake ule ule akatawala. Watu walikuwa wanamtazama kwa jicho la namna ambavyo angefeli katika ligi ya kibabe. Ligi kuu ya England. Inatajwa kwamba ni ligi bora zaidi duniani duniani kwa sasa.

PAZ 01

Pep alipofika England watu walimtazama katika jicho la kwamba alikuwa ana asilimia kubwa ya kufeli. Kwamba unapambana na watu wazito hasa. Unapambana na Manchester United, Liverpool, Chelsea na Arsenal. Ni tofauti na alipokuwa Hispania ambapo alikuwa anapambana na Real Madrid pekee.

Ni tofauti na alipokuwa na Bayern Munich. Ukiwa kocha wa Bayern Munich, hata kama ni kocha wa kawaida unakuwa na asilimia nyingi za kutwaa taji. Ni kama ilivyo kwa PSG pale Ufaransa. Kitu ambacho Pep alionekana amefeli Ujerumani ni kukosa ubingwa wa Ulaya akiwa na Bayern Munich.

Na alipotua England macho yote yalikuwa kwake. Kwanza kabisa ni namna gani ambavyo angeweza kuleta mpira wake England. Ule mpira wake wa pasi nyingi ambazo zinamfanya adui asikie kizunguzungu wakati anausaka mpira. Lakini hapo hapo namna ambavyo wachezaji wake wanakaba katika maeneo yote.

PAZ 02

Watu walikuwa wanamtazama Pep katika namna ambavyo angeweza kutengeneza ule mpira wake wa kwanza kipa anapaswa kutumia vema miguu yake pengine kuliko mikono. Mpira wake wa kwanza mlinzi wa kulia anaweza kucheza kama kiungo pale Katikati wakati mpira ukiendelea.

Pep ni wale watu wanaoitwa ‘genius’€. Hata hivyo katika msimu wa kwanza mambo yalikuwa magumu kwake. Kuna ile mechi ambayo City walichapwa mabao 4-0 na Everton kikiwa ni kichapo cha kwanza kikubwa cha Pep katika ligi tangu akiwa Hispania, kisha Ujerumani halafu England.

Katika msimu wake wa kwanza England Pep hakuondoka na taji lolote lile. Ilikuwa mara yake ya kwanza tangu awe kocha mkuu wa Barcelona kisha Bayern Munich halafu Manchester City kumaliza msimu mzima bila ya kuambulia taji lolote lile. Watu waliguna.

PAZ 03

Watu waliamini kwamba mpira wa Pep usingetoboa. Kuna kauli moja maarufu dhidi ya wachezaji mahiri wanaocheza nje ya soka la England. Huwa wanaulizwa “can you do it on a cold, rainy Tuesday night in Stoke?”. Kwamba mchezaji au kocha, hicho unachokifanya nchini kwako unaweza kukifanya katika usiku wa baridi mvua ikinyesha katika pambano dhidi ya Stoke City ugenini siku ya Jumatatu?â€

Stoke City walikuwa miongoni mwa zile timu ngumu za England ambazo zilikuwa viboko kwa vigogo. Mechi zao dhidi ya Arsenal, Manchester United, Liverpool, Chelsea na Manchester City huwa ni ngumu wakiwa nyumbani. Pep alionekana kama vile angekuwa angefeli mechi kama hizi kwa sababu hazipo Hispania.

Baada ya msimu wa kwanza kuwa wa ovyo hatimaye Pep alianza kuwatuliza waingereza. Mpira wake ukakubali na akaiteka England. Pep anaondoka England akiwa na mataji sita ya ligi kuu ya England. Kati ya hayo mataji manne alitwaa mfululizo kuanzia mwaka 2021 mpaka 2024. Hakuna kama Pep. Unaweza kupiga hesabu zake na za Sir Alex Ferguson.

PAZ 04

Sir Alex alitwaa mataji 13 ya ligi kuu ya England baada ya kutumia miaka 27 kufanya hivyo. Pep ametwaa mataji sita ndani ya miaka kumi tu. Unaweza kubashiri ni kipi ambacho Pep angefanya kama angeamua kubakia England. Inawezekana ndani ya miaka 20 tu angekuwa amefikia mataji ambayo Sir Alex alitwaa ndani ya miaka 27. Unadhani Sir Alex Ferguson alitawala soka la England? Unadhani Arsene Wenger naye alifanya hivyo? Unadhani Jose Mourinho aliwahi kutawala soka la England? Sikiliza, Pep ndiye kocha wa kwanza katika ligi kuu ya England kufikisha pointi 100 ndani ya msimu mmoja. Inakuonyesha utawala wake.

Na baada ya hapo ndani ya msimu hii kumi Pep ametwaa mataji 20 mbalimbali akiwa na Manchester City. Sio tu anaacha ufalme mkubwa ndani ya historia ya Manchester City lakini anaacha ufalme mkubwa ndani ya soka la kiingereza.

Wale waliokuwa wana wasiwasi na uwezo wa Pep kuleta mpira wa Kihispaniola ndani ya soka la Kiingereza wote kwa sasa wamenyoosha mikono. Pep sio tu kwamba amefanikiwa kuupenyeza mpira wa kihispaniola ndani ya England, lakini pia amezalisha watu wengine ambao wametawala mpira wa kiingereza kupitia mpira wake. Mfano ni Mikel Arteta aliyetwaa ubingwa wa England msimu huu akiwa na Arsenal. Ni kijana wake.

PAZ 05

Sijui Pep anakwenda wapi lakini ameishia pazuri. Ametwaa mataji mawili msimu huu na amelikosa taji la England katika dakika za majeruhi. Hakuna unachoweza kufanya zaidi ya kumsifu na kumuacha atembee kifua mbele. Alipaswa kuondoka misimu miwili iliyopita lakini akaamua kuongeza mkataba mpya. Inatajwa kwamba hii ilikuwa sababu ya kuachana na mkewe,Christina Serra ambaye alikuwa anamlazimisha Pep warudi nyumbani Hispania lakini Pep aliamua kuanzisha ‘project’ mpya ndani Manchester City baada ya zama za akina Kelvin de Bruyne kumalizika.

Hatujui kama baada ya kuamua kuachana na City na kurudi Hispania huenda ndoa ikarudi upya. Hatujui. Tunachojua ni kwamba ameondoka akiwa kifua mbele na macho mbele mita 600. Yeye ni kama Julius Caesar. Aliitazama Ligi kuu ya England kwa mbali kisha akaja, halafu akaitwaa. Ameacha alama kubwa na zaidi ameacha mpira wake pale kwa mfalme Charles. Zamani walikuwa wanapenda mipira mirefu na krosi nyingi lakini sasa hivi timu nyingi za England zinaweka mpira chini. Ni kwa sababu ya Pep.