Savinho na Spurs yaliyomo yamo?
LONDON, ENGLAND: TOTTENHAM Hotspur wametumia kiasi kikubwa cha fedha ili kumsajili Savio Moreira de Oliveira maarufu kama Savinho, ambaye ni mchezaji wa hivi karibuni mwenye gharama kubwa katika ujenzi upya wa timu unaofanywa na kocha Roberto De Zerbi.
Hata hivyo, ada ya Pauni 85 milioni aliyonunuliwa imezua maswali mengi, ingawa katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Ligi dhidi ya Charlton Athletic, Agosti 26, mwaka huu.
Itakumbukwa kwamba mechi hiyo ilikuwa dhidi ya Charlton inayocheza Championship ambapo Spurs iliondoka na ushindi wa mabao 5-1. Lakini, katika mechi iliyofuata ya Ligi Kuu England dhidi Newcastle United chama lake bila yeye ndani yake likiwa nyumbani lilikubali kichapo cha mabao 2-0, ilhali ile ya kwanza ya ligi lilikubali kipigo cha mabao 3-0 ugenini dhidi ya Brentford na sasa linaburuza mkia likiwa nafasi ya 20.
Ingawa ndiyo kwanza ligi hiyo imeanza, lakini kwa Spurs na Savinho wana mtihani mkubwa wa kujibu maswali mengi ikizingatiwa kwamba katika dirisha la usajili wa majira haya ya kiangazi ndiyo timu iliyosajili wachezaji wengi wenye majina makubwa ikitumia zaidi ya Pauni 380 milioni kuwavuta kina Omar Marmoush (Manchester City), Sandro Tonali (Newcastle United), Mateus Fernandes (West Ham United), Jan Paul van Hecke (Brighton), Marcos Senesi (Bournemouth), Andy Robertson (Liverpool) na Martin Dubravka (Burnley).
Habari kwamba Savinho hatimaye alikamilisha uhamisho kutoka Manchester City kwenda Spurs wiki moja iliyopita ilivutia hasa kutokana na ukubwa wa ada yake ya uhamisho. Inaripotiwa Spurs wameshalipa Pauni 75 milioni kama malipo ya awali pamoja na uwezekano wa kuongeza Pauni 10 milioni kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye amefanya mambo machache tangu aliposajiliwa na City kwa Pauni 30 milioni miaka miwili iliyopita.
Hiyo ni ada kubwa kupita kiasi na ni hatari kubwa kutokana na jinsi maendeleo ya maisha ya soka ya Mbrazili huyo yalivyokwama katika miezi 12 iliyopita. Lakini, kutokana na safu ya ushambuliaji kuathiriwa vibaya na majeraha, dirisha la usajili likiwa linakaribia kufungwa na machaguo mbadala kuwa machache, Spurs wako katika hali ya kukata tamaa ndiyo maana wakaamua kufanya walichofanya.
Kocha Roberto De Zerbi amehakikisha anasajili wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa Ligi Kuu England pekee wakati akikibadilisha kikosi cha Tottenham msimu huu, na kufanya hivyo kumekuja kwa gharama kubwa.
Savinho atakuwa mchezaji wa tatu kwa gharama kubwa zaidi kusajiliwa na Spurs msimu huu, lakini pia ndiye mshambuliaji wa kwanza kujiunga. Ukweli huo umeongeza nguvu ya City katika mazungumzo ya uhamisho. Kuna wasiwasi wa msingi kuhusu maendeleo yake kutokana na kucheza asilimia 31 ya dakika zilizokuwapo kwa City katika mashindano yote msimu uliopita.
Katika Ligi Kuu England alicheza asilimia 24 tu ya muda, na muda mwingi huo alikuwa akitokea kama mchezaji wa akiba katika dakika za mwisho. Alikamilisha dakika 90 mara tatu pekee katika ligi, na moja kati ya hizo ilikuwa katika mchezo wa mwisho wa msimu, baada ya mbio za ubingwa tayari kuwa zimepotea kwa Arsenal.
Kwa ujumla majeraha yalichangia, huku mfululizo wa matatizo ya misuli ya paja yakivuruga msimu wake, lakini pia hakuweza kumshawishi kocha wa City wakati huo, Pep Guardiola, kwamba alistahili kupewa nafasi zaidi, na kocha mpya Enzo Maresca pia hajashawishika na sasa ameridhia kuondoka kwake. Baada ya msimu wa kucheza kwa kiwango chini, Spurs wameamua kucheza kamari kubwa ya kifedha wakiamini kwamba Savinho anaweza kurejea kuwa mchezaji yuleyule wa awali.
Lakini, hakuna shaka kwamba wamejipatia mchezaji mwenye kipaji kikubwa. Kocha wa zamani wa Girona, Michel, alimsifu sana Savinho alipojiunga na klabu hiyo katika Ligi Kuu Italia (Serie A) Julai 2023. “Tangu Vinícius Junior alipowasili Hispania sijawahi kuona kipaji kikubwa kama hiki cha kucheza mmoja dhidi ya mmoja,” aliwahi kusema kocha huyo kuhusu winga huyo.
Kauli hiyo inaweza kuonekana kuwa imezidishwa kidogo miaka mitatu baadaye, lakini inaonyesha jinsi Savinho alivyo na ustadi mkubwa na aina ya mchezaji ambaye Spurs wanampata.
Muda wake City ulikuwa kwa kiasi kikubwa wa kutokuwa na mwendelezo, na ni jambo la kueleweka alihukumiwa kutokana na msimu wake wa 2025-26 uliokuwa wa kukatisha tamaa, ambapo alifunga bao moja na kutoa asisti moja katika dakika 821 kwenye Ligi Kuu England.
Lakini, msimu wake wa kwanza wa 2024-25 akiwa City ulikuwa wa kukumbukwa zaidi, na takwimu zake za msimu huo zinatoa matumaini zaidi kwa Spurs alipofunga bao moja, lakini alitoa asisti nane licha ya kucheza dakika 1,773 kati ya 3,420 kwenye mashindano hayo.
Asisti zote nane pia zilitokana na mchezo wa wazi, huku wachezaji watano pekee wakitoa nyingi zaidi yake. Lakini, miongoni mwa wachezaji aliowazidi kwa asisti za mchezo wa wazi msimu huo ni Cole Palmer (7), Bruno Fernandes (7), Eberechi Eze (7), Enzo Fernández (6) na Morgan Gibbs-White (6), na kila mmoja kati ya wachezaji hao alicheza angalau dakika 900 zaidi ya Savinho.
Kwa kuzingatia kila dakika 90, alishika nafasi ya tatu kwa asisti za mchezo wa wazi (0.41 kwa kila dakika 90), huku Mohamed Salah pekee aliyekuwa Liverpool (2.3) akiwa na wastani mkubwa zaidi wa nafasi alizotengeneza kwa kila dakika 90 (2.2).
Ni muhimu kutambua kwamba asisti tatu kati ya hizo alizitoa dhidi ya timu ambazo baadaye zilishuka daraja, lakini pia alitengeneza mabao katika mechi za nyumbani na ugenini dhidi ya Arsenal.
Kwa kuwa ni mchezaji anayetumia mguu wa kushoto, ni jambo la kawaida kudhani kwamba anakuwa vizuri zaidi upande wa kulia, akikatiza ndani ili kutishia lango, lakini kutokana na kurejea hivi karibuni kwa winga wa kwanza wa upande wa kulia Spurs, Mohammed Kudus, huenda hii isiwe nafasi ambayo Spurs wanamhitaji zaidi Savinho.
Mchezaji huyo yuko vizuri vilevile upande wa kushoto. Aligawanya muda wake City kwa usawa kati ya pande zote mbili, lakini alijijengea jina Girona akicheza upande wa kushoto. Anaweza kuanza Spurs na uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali muhimu vyovyote vile.
Tishio lake kubwa hutokea anapokuwa na mpira miguuni, akikimbia dhidi ya mabeki na kutafuta kuwaandalia wengine nafasi. Katika Ligi Kuu England 2024-25, Jeremy Doku, Kudus na Julio Enciso pekee walikamilisha chenga nyingi zaidi kwa kila dakika 90 kuliko Savinho (2.6). Na kati ya wachezaji 10 bora waliojaribu kupiga chenga, Doku pekee (asilimia 60.5) alikuwa na kiwango bora kuliko Savinho (51.0%).
Lakini, siyo lazima kila mara amzidi mpinzani kwa chenga ili awe na athari. Miongoni mwa wachezaji waliocheza angalau dakika 1,000 katika Ligi Kuu England msimu wa 2024-25, Doku pekee (11.6) alikuwa na wastani bora zaidi wa kukokota mpira mbele kwa angalau mita 10 kwa kila dakika 90 kuliko Savinho (6.8), huku pia akiwa kileleni mwa ligi kwa kufanya hivyo na kufuatiwa na kutengeneza nafasi, akiwa na 1.3 kwa kila dakika 90.
Son Heung-min pekee aliyekuwa Spurs alimaliza kwa kukokota mpira na kisha asisti (0.30 kwa kila dakika 90) mara nyingi zaidi yake (0.25). Pia alifanya vizuri katika kukokota mpira na kumalizia kwa shuti, akiwa na jumla ya 28 kwa kiwango cha 1.4 kwa kila dakika 90 (cha tatu bora katika ligi hiyo), lakini hakufunga hata bao moja kutokana na nafasi hizo.
Mbrazili huyo amekuwa akishindwa kutoa matokeo ya mwisho linapokuja suala la mabao katika maisha yake yote ya soka. Mbali na kufunga mabao tisa akiwa Girona 2023-24 katika Serie A, hajawahi kufunga zaidi ya bao moja katika msimu mmoja wa ligi. Mabao mawili katika misimu miwili ya ligi kwa timu iliyotawala mpira kama City ni kiwango duni cha uzalishaji, hata kwa kuzingatia muda wake mdogo wa kucheza.
Itakuwa muhimu kwa Tottenham Hotspur kwamba mchezo wake wa asili siyo kutafuta tu kupokea mpira miguuni na kukimbia nao.
Hilo ndilo alilopewa jukumu la kufanya chini ya Guardiola huko City, lakini pia anapenda kukimbia nyuma ya mabeki, na alifanya hivyo kwa ufanisi mkubwa Girona, mara kadhaa akikimbilia mipira ya kupenyezwa kabla ya kuipiga pembeni kwa mshambuliaji wa kati, Artem Dovbyk kufunga wakati huo.
Mshambuliaji anayekimbia nyuma ya mabeki ni aina ya mchezaji ambaye Tottenham wamemkosa tangu walipompoteza Son na na pamoja na upungufu wake Brennan Johnson.