Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys ina deni moja la mwisho

SERENGETI Pict

Muktasari:

  • Katika mashindano hayo ya kuwania kufuzu AFCON U17, ambayo yalihusisha timu kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika (CECAFA), Serengeti Boys ilipata ushindi katika mechi zote kuanzia ya kwanza ya makundi hadi fainali.

TIMU yetu ya taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imetuheshimisha vilivyo kule Ethiopia ambako ilikuwa ikishiriki mashindano ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo (AFCON U17) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.

Katika mashindano hayo ya kuwania kufuzu AFCON U17, ambayo yalihusisha timu kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika (CECAFA), Serengeti Boys ilipata ushindi katika mechi zote kuanzia ya kwanza ya makundi hadi fainali.

Kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ya kuwania kufuzu AFCON U17, bila kupoteza mchezo huku ikifunga zaidi ya mabao mawili katika kila mchezo, ni uthibitisho kwamba Serengeti Boys ilikuwa ni timu bora zaidi katika mashindano hayo.

Haikuishia kwa timu kutwaa ubingwa bali pia hata wachezaji baadhi mmoja mmoja na kocha wao Elieneza Nsanganzelu walitwaa tuzo binafsi kutokana na mchango wao mkubwa walioutoa katika kuwezesha mafanikio ya timu hiyo.

Hata hivyo, kwa niaba ya washkaji hapa kijiweni, tunawakumbusha Serengeti Boys kuwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya kufuzu kupitia kanda ya CECAFA na kupata tiketi ya kucheza fainali za Afrika, haipaswi kuwafanya wabweteke na kujiona wameshamaliza kazi.

Hicho ni kiunzi cha kwanza tu ambacho wamekiruka, lakini kuna cha pili ambacho ni kigumu na muhimu zaidi nacho ni kufanya vizuri katika Fainali za AFCON U17 ili Serengeti Boys iweze kufuzu Kombe la Dunia.

Na kama wakituliza akili, kibarua hicho cha kuwania kufuzu Kombe la Dunia hakitoweza kuwa kigumu kwao kwa sababu hivi sasa Afrika inatoa wawakilishi 10 katika Kombe la Dunia la Vijana wa umri huo.

Maana yake Serengeti Boys ikifanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo ya AFCON U17, itakuwa imeshajihakikishia moja kwa moja kufuzu Kombe la Dunia pasipo kutegemea kupenya kwa kupitia nafasi mbili za besti luza.

Wakifanikiwa kwenda Kombe la Dunia watakuwa wametimiza kwa kiasi kikubwa malengo yetu. Sio lazima watwae ubingwa.